INTERPREFILM COURSE

- Utunzi na uandishi wa story (Screenwriting)
- Uigizaji na Upangaji wasanii (Acting & Casting)
- Uzalishaji na Uongozaji (Producing & Directing)
- Ubunifu wa Sauti (Sound Designing)
- Upigaji Picha (Cinematography)
- Uhariri wa Sinema (Editing)
- Masoko (Marketing)

WAKATI WA MAFUNZO

- Mwanafunzi atapatiwa kitambulisho, T-shirt maalumu na kukutanishwa na wadau na wasanii wakubwa ili kupanua uelewa wake.

BAADA YA MAFUNZO

- Itafanyika filamu ya mafunzo kwa vitendo (Practical Film) kuthibitisha uelewa wa mwanafunzi.
- Vyeti vya uthibitisho vitatolewa kwa wote.
- Msanii kuajiriwa na kampuni wasimamizi, wadau au kujiajiri mwenyewe!
MUDA WA KOZI: Miezi mitatu (3)
KUANZIA: Tarehe 21/01/2011
FORM ZA KUJIUNGA ZINAPATIKANA KWA Tsh.5,000/= katika ofisi ya Kwanta Teknolojia (Internate Cafe), Kinondoni, Muslim, jirani na Baclays Bank, Mate Barbar Shop, Ubungo Riverside na IFA Tanzania, Jengo la Clock Tower Trading Center, Mnzi Mmoja.
Au piga simu namba 07141696655.

Mtandao ni www.ifatanzania.blogspot.com

Wote mnakaribishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Tunahitaji pia mafunzo juu ya uhakiki wa filamu. Filamu za Bongo zina hadithi ile ile: Mtu mmoja mwenye shida anafadhiliwa na mtu mwingine mwema. Halafu aliyefadhiliwa anamsaliti mfadhili wake. Kilema cha kutegemea ufadhili na kukosena kwa hadithi anuwai, ni kasoro katika filamu zetu. Lazima tupige hatua zaidi.

    ReplyDelete
  2. Ebana hii kitu ni bure kweli, mbona alafu wanadai Tsh 5,000.00.
    Kama ni bure sema bure na kama kuna kulipia semeni ukweli.

    ReplyDelete
  3. screen writing au script writing? nyie wenyewe mnachemsha hivyo sasa mtawafundishaje wengine???

    ReplyDelete
  4. Wa bongo kwa kukosos. Wengine sijui mlisoma enzi za mkoloni na kukalia kukariri kidhungu cha dictionary? Hapo huyo aliyesema screenwritting hajakosea chochote. Kabla hujakosoa mtu kajifunze kwanza. na hao wanaolalamika ati 5000? Mumeambia mafunzo ya bure lakini hizo elfu tano labda ni administration fee. Unajua ni wangapi wanaweza kwenda tu kwa vile ni bure na kutofuatilia au kumaliza mafuzo? Mtu kajitolea kuwapa knowledge chukueni. Huwezi jua utaiihitaji hiyo knowledge lini. Mimi sipo bongo na wala hii sio career yangu lakini ningekua bongo nikwenda na kujifunza kama muda uko.

    Acheni longolongo mkipewa knowledge tumieni na mshukuru. Ulimwengu wa leo hutakiwi kukaatu na field moja huwezi jua soko la ajira litahamia wapi?

    ReplyDelete
  5. @ anonymous 12:34 pm just FYI. Screenwriting is the art and craft of writing scripts for film, television or video games. If you have nothing good to say don't say anything...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...