Lilian Chengula, aliyekuwa mhasibu wa Shirika la Umeme nchini, (Tanesco) amesomewa mashitaka 85 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidaiwa kuiba fedha za mwajiri wake Sh bilioni 1.3.

mbele ya hakimu Mustapha Siani alisomewa mashitaka 84 ya wizi na shitaka moja kati ya mashitaka hayo la uhujumu uchumi.

Alidaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2009 hadi Septemba 2010 katika ofisi za shirika hilo wilaya ya Kinondoni akitumia nafasi yake ya uhasibu.

Chengula alisomewa mashitaka na mwendesha mashitaka Inspekta wa polisi Ema Mkonyi, Zuberi mkakati, na Beatrice mpangala kwa kupokezana. Alidaiwa akilikuwa akiliibia shirika hilo kwa kutumia vocha alizokuwa akiziwakilisha kwa nyakati tofauti.

Aidha katika shitaka la uhujumu uchumi mshitakiwa alidaiwa kusababisha hasara kwa mamlaka iliyowekwa kisheria ambayo ni mwajiri wake Sh 1,312,717,717.70 kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.

Mshitakiwa alikana mashitaka yote isipokuwa la uhujumu uchumi ambalo mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza isipokuwa kwa kibali toka kwa mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu lolote kwasababu haikuwa imepewa kibali. Mahakama hiyo itatoa maamuzi juu ya dhamana ya mshitakitakiwa kesho na amerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hii ni move ya kupooza wananchi from what is really going on in the country. We need BIGGER FISH, hawa ni vi dagaa.

    ReplyDelete
  2. Safi sana mhasibu wangu, ukitaka kula nguruwe, chagua aliyenona.
    Ningeshangaa kusikia unashitakiwa kwa kukwapua laki mbili. Wa- TZ tunajua wengine wanataka kukwapua Bilioni 94 KWA KUTUMIA CHOMBO HICHOHICHO CHA SHERIA.
    Kila atakayejipendekeza mkatie kidogodogo na watakuachia kwa ulaini tu.

    Abiola Jr.

    ReplyDelete
  3. Maaaama namfahamu huyu. Jamani never say never...Lakini kosa sio lao. Wameona huko juu wote wanakula wanavyotaka na wao wameiga.

    ReplyDelete
  4. Kula nkula vibaya kukomba mboga.
    wale wa EPA na Radar waliishia wapi?

    ReplyDelete
  5. Pole sana dada Lilian. Hii ni kidogo sana na mungu atakusaidia. Kwanza wewe peke yako huwezi kuchukua hizo hela na itahitaji proof lakini kwanini ushitakiwe kwa kosa la uhujumu uchumi na mbona wale jamaa walikwapua bilions of money za Benki kuu walipewa kesi ya kawaida. Pole sana maana Tanesco wamepoteza billions za dowans na sasa wanakamata wadogo ili kuonesha wanafanya kazi.
    John wa DSM

    ReplyDelete
  6. Uncle tunaomba uwe unatoa na picha ya mhusika pengine tunmjua kwa jina tofauti tusije tuka acha kumpa mpole. After all kesha shtakiwa nasi tumjue.

    ReplyDelete
  7. Da hii kali sasa kila mtu hii bongo anawaza kuiba, kwa hiyo limekua Taifa la wizi, halina hata mpangilio, tatizo wanaoumia walala hoi , ambao hawana sehemu ya kuiba. Hii hapana jamani inasikitisha kwa watu wasipata hizo sehemu za kuiba,Inaonekan ni Taifa la wezi lisilokua na mwelekeo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...