Katibu Mkuu Wizara ya Maji Injinia Christopher Sayi (katikati) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani KFW kanda ya Afrika Dr.Muller (wa kwanza kulia) kuhusu Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji alipotembelea Wizara ya Maji.Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa KFW hapa Tanzania Dr.Wolfgang.

Raisi wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani KFW kanda ya Afrika Dr.Muller ametembelea Wizara ya Maji na kupata taarifa juu ya utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Setka ya Maji

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Programu hiyo ya Maji, Katibu Mkuu Wizara ya Maji Injinia Christopher Sai alimueleza Raisi huyo kuwa,kwa niaba ya Serikali wanalishukuru Shirika hilo kwa kuwa moja ya wachangiaji wakubwa wa Programu ya Sekta ya Maji kwa ujumla. ‘’Ni matumaini yetu kuwa mtaendelea kutufadhili hata baada ya awamu ya kwanza kwisha’’ alsema Katibu Mkuu huyo.

Alifafanua kuwa, awamu kwanza ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji inaendelea vizuri pamoja na kuwa na changomoto mbalimbali. Kwa upande wake Mkurugenzi huyo wa KFW kanda ya Afrika alisisitiza sula zima la matumizi bora rasilimalifedha kwa miradi husika na mfumo mzima wa kutoa taarifa ili Shirika hilo liendelee kufadhili Progarmu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji.’’

Tuanahijitaji mfumo mzuri wa kutoa taarifa ya matumizi ya fedha kwani wafadhili suala hili ndio msisitizo wao mkubwa’’ alsema Dr Muller. Akijibu hoja hiyo, Katibu Mkuu alimuelza Dr Muller kuwa tayari Wizara kupitia kitengo chake cha TEKNOHAMA imeatayarisha progaramu ya mfumo wa habari itakayoziunganiasha Halmashauri zote na wadau wa Programu Maendeleo ya Sekta ya Maji kupata taarifa za Matumizi ya fedha, zabuni mbalimbali, pamoja na malipo yatakayofanywa kwa wakandarasi kwa Miradi yote ya Sekta ya Maji nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...