Wengine wakiwa wana furahia mvua wangine imekuwa ni kilio kama inavyoonekana hapa barabara ikiwa imezibwa na mti ulioanguka jirani na hoteli ya Southern Sun jijini Dar jana. Chini ni gari iliyoangukiwa na mti huo
Mti waangukia gari lililoegeshwa nje ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM jijini Dar kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali jana. Miti karibu yote katikati ya jiji ni ya toka enzi za mkoloni. Kuna haja wazee wa Jiji wakaliangalia hili kwa jicho la kuondoa miti yote iliyokwisha zeeka na kupanda mipya badala yake.
Wananchi wanao tumia maegesho chini ya miti jijini Dar wanatakiwa kuwa makini kwani miti mingi sasa imezeeka, na ukichukulia hali yamvua ambayo inaambatana na upepo mkali athari na hasara kwao ni dhahiri kama mdau mwenye gari hili anavyodhihirisha. Picha na mdau Christopher Mfinanga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Kuondoa miti na kupanda mipya sio sahiiiiiii!!

    Kuna wataalamu wa miti,watumie njia za kuhakikisha madhara hayatokei.
    kuiondoa ni kuleta madhara kwa mazingira, juhudi zinafanywa kutunza miti ya asili kwa kupunguza matawi kuepuka janga kama hilo.

    Tusiropoke bila kufikiaria, na tusiangalie maslahi yetu tu, miti inatunzwa ili idumi karne na karne. Tatizo uzembe mwingi TZ wizari na voingozi miji husika wawajibike

    ReplyDelete
  2. Hiyo miti iliyopo hapo katikati ya mji haishughulikiwi kwa kukatwa matawi na kadhalika kwa hivyo hayo ndiyo matokeo.

    Ijapokuwa mimi siyo mtaalamu wa miti lakini kwa maoni yangu hiyo miti ina matatizo kwani nadhani mizizi yake haikwenda very deep labda kwa sababu fulani (soil type na kadhalika) kwa hivyo imekaa kihasara hasara hivi. Na hasa ile mivinje iliyooteshwa barabara ya baharini (Ocean Road)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...