Wadau naomba msaada wa mawazo na
ushauri kwa tatizo linalomkabili binti yangu.

Binti yangu mwenye umri wa miaka minane (8) anakabiliwa na tatizo la kujisaidia haja ndogo akiwa amelala kitandani usiku. Anaweza kujisaidia mara moja, mbili na wakati mwingine hata mara tatu kwa usiku mmoja, yaani hawezi kabisa kujizuia wala hajitambui anapokuwa usingizini.

Nafahamu kwamba watoto huwa na tatizo kama hili wanapokuwa wadogo, lakini binti wa miaka minane anapaswa kuwa tayari awe na uwezo wa kujidhibiti mwenyewe.

Niliwahi kupewa ushauri wa kumpunguzia vyakula vya maji maji na vinywaji usiku bila mafanikio, pia nimejaribu kumuamsha mara kadhaa kumtoa usiku kwenda kujisaidia, lakini mara tu anapotoka kujisaidia, akirudi kulala akakojoa tena usingizini.

Nina watoto wengine walio chini ya umri huo na wengine wenye umri zaidi ya huo, na hawana tatizo hilo, tena ndani ya miaka miwili tu waliacha kukojoa kitandani. Kimasomo anafanya vizuri sana, nina wasiwasi kwamba akiendelea na tatizo hili linaweza kumwathiri kiakili na hatimaye kuathiri maendeleo yake kimasomo.

Kupitia hapa nitashukuru sana kupata ushauri na mawazo kutoka mtu yeyote mwenye ujuzi, uzoefu au aliyewahi kupatwa na tatizo kama hili na akafanikiwa kulitatua.

Asanteni sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Nadhani binti yako si kwamba ana tatizo...ila kwa uzoefu nimeona mabinti wengi wakikojoa kitandani hata walipokuwa tayari wako kidato cha kwanza na baadaye waliacha kabisa baada ya muda. Nadhani hili ni suala la kibaolojia ambalo kuna vitu vinaitwa sphincters (mwone Dk kwa ushauri zaidi)...ambazo zinakuwa hazijakomaa sawasawa ili kusaidia mkojo usipite hovyo. Hivyo hivyo kadiri atakapokuwa anakua..hizi sphincters zitakuwa zinakomaa hadi anaweza kuzibana na kuzuia asijikojolee tena. So maoni yangu umwone Dk akufafanulie kuhusu suala hili na utaelewa kumbe ni kitu kidogo sana. Mtumishi

    ReplyDelete
  2. Ndugu pole na hili tatizo ingawa mimi siyo mtaalam wa mambo haya ili jambo ni lakawaida kwa watoto wadogo wala usiogope chamsingi wewe kuwa unamjari unambembeleza usimgomee ukianza kumtisha tisha anaweza kuasilika kisaikolojia wewe kawaone wataalam hosptali yeyote ile pengine watakusaidia na tuone wachangiaji wengine watasemaje,

    ReplyDelete
  3. This problem is very common
    Wataalum waita tatizo hilo...nocternal enuresis
    Mpeleke huyo mtoto kwa daktari mwenye ujuzi wa maradhi ya watoto...paediatrician.
    Now I will tell you what you should not do
    Kwanza usimpige au kumgombesha au kumtisha aina yeyote
    Do not diturb her sleep kama unavyosema, that will impair her school work
    Tulipokuwa wadogo jamaa hao tuliwaita VIKOJOZI
    Tuliruhusiwa kuwapaka majivu na kuwaimbia
    KIkojozi kakojoa na nguo kazitia moto
    Nifikiri tabia hizo haziendelei siku hizi

    Wakatabahu (DCH,,Dublin)

    ReplyDelete
  4. Nimesoma na watu boarding sekondari mpaka form 1-2 (miaka 15-16) bado walikua na tatizo hili. Hivyo, ingawa nakubaliana na wewe kuwa amepitiliza umri wa kuacha kukojoa kitandani, nadhani bado una muda wa kumsaidia kutatua tatizo hilo, nakupa moyo,
    hata hivyo sina ujuzi wa kitaalamu juu ya hili, wadau tusaidieni,

    ReplyDelete
  5. Wala hauko peke yako mdau. Angalia dondoo hizi kwa tatizo hili liitwalo BEDWETTING. Bedwetting - Solutions that Work for Child Bedwetting: A Guide for Parents
    Most doctors consider a bedwetting child to be any girl older than age four and any boy over age five who wet the bed. Bedwetting generally declines with age. About 10% of all six year olds and about 3% of all 14 year olds wet the bed. In a very small number of cases, bedwetting can continue into adulthood. Bedwetting (enuresis) is considered to be PRIMARY if the child has never been dry at night or only is occasionally dry at night. SECONDARY enuresis refers to bedwetting episodes that occur after a child has been dry at night for a considerable length of time.
    Primary Enuresis: This is the main topic for this page and will be considered in depth. When the problem continues into the school years, appropriate intervention can usually correct the problem. This page will review the causes and treatments for Primary Enuresis.
    Secondary Enuresis: Children who have been dry at night for a considerable period of time may have occasional episodes of bedwetting. These are usually related to stresses in a child's life and clear up on their own. Three of the more common events likely to cause bedwetting in young children are: hospitalization, entering school and the birth of a sibling. Children can also experience stress from such family problems as divorce, parental alcoholism, financial pressure as well as abuse and neglect. If the symptoms persist, you should consult your child's doctor because the cause may be a physical problem which may require diagnosis and treatment.
    Primary Functional Enuresis (Chronic Bed-wetting)
    Cause: Chronic bed-wetting is thought to be related to (1) a physically and/or neurologically immature bladder and/or (2) a deep sleeping pattern. Apparently these children often sleep so deeply that they are not aware of the message the bladder sends to the brain saying it is full. It is presumed that bed-wetting is an inherited condition. Usually a parent, aunt, uncle, grandparent or other family member(s) will have had the condition. Also, children with attention deficit disorder, learning disabilities or allergies seem to be more likely to be bed-wetters than children in the general population..
    Treatment:
    First of all, almost all children outgrow their bed-wetting habit. As children mature, their muscles become stronger and their bladder capacity increases. They tend to sleep less deeply and to become more sensitive to messages the bladder sends to the brain. There are two approaches to treatment: Medical or Behavioral. The medical treatment usually consists of the use of one of two drugs:
    Imipramine (Tofranil) This drug is a tricyclic antidepressant. It is thought to either improve the child's sleeping pattern to improve the functioning of the smooth muscles found in the bladder. This medication brings some improvement to about 30% of the children who have tried it. Often, the symptoms return when the medication is discontinued. The drug can cause serious side effects and needs to be closely monitored by the prescribing physician.
    Desmopressin acetate This drug is a synthetic form of the antidiuretic hormone and is administered as a nasal spray. It helps the child's body make less urine, and thus lessens the risk that the child's bladder will overfill during sleep. The medication often works quickly. However, the condition may return after discontinuation of it's use. While this medication is much safer than Imipramine, it still can cause some side effects.
    Mdau Dr Chacha Mwita, London

    ReplyDelete
  6. Hili tatizo linakwisha ila tafadhali mpigie mtu anayeitwa Mr Katondo kwenye number 0652960055, kitu cha muhimu cha kuzingatia sio biashara, ila kwa ushauri nasaha na kukuelezea vyakula gani ale na vipi asile mpaka tatizo litakoisha. ila zingatia ushauri ni bure sio Biashara, usiogope.

    ReplyDelete
  7. Mimi nafikiri ungewaona wataalamu wa afya (madaktari) wangekusaidia zaidi.

    ReplyDelete
  8. Kuna hii dawa ya kienyeji mfanyie kikawaida sisi waislam mtu anapokufariki humuosha na yale maji yake tukiomuoshea huwa tunayafikia pale juu tukishayafukia huwa ni udongo na maji maji kidogo basi hapo juu huyo mtoto wako avue nguo zake zote na umburute hio sehemu iliyofukiwa ya maji ya mfu .....inasaidia na ataondokewa na hilo tatizo ndugu yangu mara moja mimi watoto wangu wawili walikuwa na hilo tatizo na sasa hivi limeondoka kwa hio dawa ya kienyeji

    ahsante sana

    ReplyDelete
  9. Kikojozi MstaafuFebruary 07, 2011

    Ah kawaida hiyo akikua ataacha. Mi ni mwanaume ila nakumbuka mara ya mwisho nimekojoa kitandani nilikuwa na miaka 24.

    Nilipokuwa mdogo ilikuwa inatokea mara kwa mara zaidi. Ila kadiri umri unavyoongezeka inakwenda ikipungua.

    Na mikojo yote inakuja kupitia ndoto. Naota niko mahali nakojoa then huku pasi kujijua nakojoa kweli kitandani. Then as joto na unyevunyevu wa mkojo unaponigusa nashtuka. Sometime naweza kuwahi kuzuia usimwagike zaidi. Sometime nashtuka too late mkojo wote ushatoka umeishia kwenye godoro.

    Ni aibu of course, ila utafanyeje? Nakumbuka enzi niko bweni siku nikijikojolea najisikia hovyo kweli halafu naona noma room mate wakijua.

    Njia nilizokuwa natumia kuzuia hali hiyo isitokee ni kunywa vimiminika kidogo sana usiku na kukojoa kabla ya kulala.

    Ila siku nikijisahau nikanywa maji mengi au chai usiku basi nalala kwa machale.

    Siku nimekojoa when I was 24 (my last time) nilikuwa nimetoka club kwa hiyo nimekunywa bia kadhaa. Ilikuwa noma kinoma maana nilikuwa nimelala na demu wangu na ndio siku hiyo akajua mi kikojozi.

    Sema it was the only time nimekojoa nikiwa naye na hapo tulikuwa tushalala pamoja on same bed for 8 months. Kwa hiyo nikajitahidi kuua soo kwamba nilikuwa nimelewa sana. Ila ndio hivyo mpaka kesho huwa ananitaniaga Kikojozi!

    Lakini sasa hivi nina miaka 30 na sijajikojoelea usingizini tena toka umri huo wa 24. Yaani siku hizi hata ninywe bia sita kabla ya kulala nalala FRESH tu sijikojolei mpaka asubuhi.

    Kwa hiyo I believe your daughter will get fine with age. Ila ndio hivyo azoee kuitwa Kikojozi.

    ReplyDelete
  10. Habari ndugu
    Mimi pia mtoto wangu wa miaka 7 alikuwa na tatizo hilo hilo, nikaenda hadi mahospital wakamcheck Diabetes na mambo tele lkn hajaonekana na tatizo lolote. Sasa mimi mwenyewe nimework out system kuwa akienda kulala namkumbusha kwenda kukojoa na baada ya one hour or two namuamsha kwenda kukojoa tena. Usimuonee huruma ukasema "oooh, kaenda kulala sasa hivi, nitamkatia usingizi". Ukimuonea huruma tu, ukasema acha alale kidogo, ukienda kashalimwaga. Na ukienda kulala wewe mwenyewe kama two hrs after muamshe tena. Huna haja ya kuamka usiku wa manane kumtoa tena. Jaribu hivyo, nategemea itasaidia sana. Mimi binafsi imesaidia, mtoto wangu hakojoi tena kitandani kabisa.
    And No Harm in Trying.
    Kila la Kheri Inshaallah

    ReplyDelete
  11. Mimi ni mwana ume miaka 36 nilikuwa na tatizo hili mpaka nikiwa na miaka ya 20 hivi sijapewa dawa wala nini. Inawezekana sio siriasi sana; haiihitaji matibabu. Yeyeye mwenyewe akiwa mkubwa ataona ni nuhimu sana kujizuia kula/kunywa vyakula vya majimaji wakati wa jioni...Maombi pia yanasaidi."Yeye mwenyewe aliuchukua udhaifu wetu na kuyatwaa magonjwa wetu"...

    ReplyDelete
  12. mimi pia mtoto wangu alikuwa na tatizo hilo lakini hivi sasa hana tena baadaya kumuona daktari, je mtoto wako anakoroma? najaribu kukuuliza maswali ili kujaribu kuona ikiwa ugonjwa unafanana kabisa na mwanangu basi nikupe muktasari wa habari pembeni ya ukumbi, na ikiwa ujisikii vyema ukumbini hapa, basi wasiliana nami kupitia michuzi.

    ReplyDelete
  13. habari ndugu yangu na pole kwa hilo.
    mimi ninakushauri uende hospitali mtoto akafanyiwe uchunguzi zaidi ikiwa ni pamoja na kipimo cha sukari. Dalili moja wapo ya ugonjwa wa sukari kwa watoto especially wa umri huo ni kukojoa kitandani na kulala sana (kushindwa kuamka mapema kwa hiari) pia huwa wanachoka sana. wanapungua uzito ghafla na kuongezeka ghafla pia.

    ReplyDelete
  14. Kama walivyosema wengine mpaka kwenye form1 utakuta watoto wengine bado wanakojoa kitandani usiku. Usiwe mkali na yeye bali jaribu kumsaidia kadri uwezavyo. Labda asinywe fluids nyingi near bed time na pia jaribu kuweka check point ambapo wewe utaamka kwenda kumpeleleka kujisaidia

    ReplyDelete
  15. Pole sana mdau,mimi nadhani mwanao ana kisukari ambacho huchangia sana mtu kukojoa kitandani usiku au hata mchana bila kujitambua,kwa hiyo nashauri mpeleke hosipitali pia kuna tiba za kienyeji/asili,kwetu sisi kama mtoto anakojoa unafanya timing wakati ng'ombe anazaa kwa mara ya kwanza ktk maisha yake kabla ndama hajagusa chini yaani akishatoa miguu tu mwanao awe karibu ang'ate kidogo mgoo wa ndama tatizo lake litaisha

    ReplyDelete
  16. Mdau hata mimi mtoto wangu anakaribia 8 years bado anakojoa ingawa mara moja moja kuna wakati anafululiza na wakati mwingine hakojoi, nadhani umri bado ukiweza ni kumwamsha tu na kumpeleka kukojoa.Watu tumekojoa hadi umri mkubwa tuko kwenye ndoa!!! inatokea mara moja kwa miaka!!! ila angekuwa kwenye miaka ishirini hivi na anakojoa kila siku nadhani hiyo inakuwa tatizo.
    Mama wawili.

    ReplyDelete
  17. Mimi nikiweka comment yangu michuzi ataibania hasa huyo wa dawa ya kienyeji nilikuwa na maswali. Ina maana inabidi asubiri hadi kuwe na kilio mahali ama pale yalipofanyika hayo mambo zamani??!!

    Observer

    ReplyDelete
  18. Ukikwama kupata jibu huko hospitali basi soma kwenye internet au omba mtu akupee maelezo kuhusu acupuncture. Tahadhari hii ni tiba ya kichina lakini Tanzania kuna wachina matapeli chunguza walio halali.Sikuhizi kuna vipindi vingi kwenye tv ambavyo huonyesha kuhusu hii tiba, binafsi ninao mfano wa karibu kabisa kabisa wa matatizo mbalimbali ya mwili wabinadamu.

    ReplyDelete
  19. mimi sina ujuzi ila nikiwa bongo niliwahi kumuona msichana mkubwa mwenye tatizo hilo mwenyewe aliamini ni ugojwa akitafuta dawa bila mafanikio.
    nimekuja huku ulaya nilipata kibaruwa cha kuangalia watoto wa mama mmoja ambao walikuwa watatu ote wa kike umri wao ni 9,6,4 huyu mkubwa alikuwa anakojowa na mdogo wao wa mwisho hivyo basi kama kungekuwa nadawa hawa watoto wangetibiwa kwani sidhani kama bongo wanawataalamu kuzidi hapa.
    tena huyu mama kashazoea kabisa huwa anawapa nepi(pampers)mimi nadhani huenda ikawa njinzi (magonjwa ya kuridhi) usianze kumpa mtoto makolokolo ila mtafutie mpila mkubwa ili asiharibu godoro lake na usikubali watu wakamnyima raha akikuwa atajiangalia mwenyewe na bahati nzuri bongo kunajuwa akikojowa anazitia kwenye maji ya omo anazianika na usiku anazitumia tena siku zinakwenda na mfundishe yeye mwenyewe kujihudumia ili isiwakele watu wa karibu yake.

    ReplyDelete
  20. Mimi ni mwanamke mwenye miaka 30 na nilikuwa nakojoa kitandani hadi miaka 11 tena wadogo zangu nilio wazidi zaidi ya miaka mitato wala walikuwa hawakojoi kitandani, niliacha mwenyewe tu nikiwa na umri wa miaka 12 (darasa la tano hapo)wala wazazi wangu walikuwa hawaniamshi usiku kwenda chooni, mama yangu alikuwa ananikumbusha kuanika godoro nje kabla sijaenda shule, hicho kitendo cha kuanika godoro nje kila siku ndicho kilinifanya nitamani kuacha kukojoa. Ushauri wangu wala usihofu mtoto wako bado mdogo ataacha tu.

    ReplyDelete
  21. Pole sana MDAU ulioleta hii mada,dawa ni ndogo sana unachotakiwa kufanya siku ambayo atafanya tukio hilo nikimaanisha akijikojolea kitandani wewe asubuhi mtembeze mitaani huku watoto wenzake wakimuimbia wimbo wa "KIKOJOZI" nina uhakika hatorudia tena kukojoa kitandani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...