Tangazo rasmi limetolewa kuthibitisha kuwa Rais Museveni ndiye mshindi katika uchaguzi uliofanywa Ijumaa.
Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Yoweri Museveni alishinda kwa asilimia 68, katika uchaguzi huo uliofanyika Ijumaa, naye mpinzani wake mkuu Kizza Besigye alipata kura asilimia 26.
Bw Besigye amekataa kukubali matokeo hayo na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika shughuli ya uchaguzi.
Chama kilicho madarakani kimetuhumiwa kwa kutumia rasilmali ya serikali kuwahonga wapigaji kura.
Uchaguzi huo uliendelea kwa utulivu ingawaje kuna ripoti za vurugu kadhaa baina ya wafuasi wa chama kinachotawala na chama cha upinzani.
Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Yoweri Museveni alishinda kwa asilimia 68, katika uchaguzi huo uliofanyika Ijumaa, naye mpinzani wake mkuu Kizza Besigye alipata kura asilimia 26.
Bw Besigye amekataa kukubali matokeo hayo na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika shughuli ya uchaguzi.
Chama kilicho madarakani kimetuhumiwa kwa kutumia rasilmali ya serikali kuwahonga wapigaji kura.
Uchaguzi huo uliendelea kwa utulivu ingawaje kuna ripoti za vurugu kadhaa baina ya wafuasi wa chama kinachotawala na chama cha upinzani.
Museveni naye angeachia ngazi. Yale yale ya Idd Amin atayarudia. Hizi power zinashida sana.
ReplyDeleteJamani, huu sasa ni upuuzi. Kumbukeni mwaka 1986 wakati Museveni alipokuwa maporini Uganda, aliwahi kuhojiwa na BBC News World kwa nini anataka kuchukua urais, na kwa nini mpaka aende porini kwa kutumia watoto? Yeye (Museveni) alijibu watoto ni taifa la kesho na ataka kuikomboa Uganda kwa ajili ya hiyo. Pia akaelezea kuwa tatizo la Afrika kuwa na mchafuko wa siasa/mapinduzi ya mara kwa mara ni kutokana na vingozi kukaa madarakani muda mrefu na yeye hatarajii kufanya hivyo. Je, tuseme kajisahau au madaraka ni matamu zaidi? Tukumbuke kuwa kukaa madarakani zaidi kama vile Mubarak, Mugabe, Mobutu na baadhi ya viongozi wengine barani Afrika kuna haribu hata muelekeo wa nchi. Angalieni zimbabwe kwa mfano. Miaka ya mwanzoni ya themanini ile nchi iliweza kulisha Afrika nzima ila sasa wananchi wake wanakuja TZ kuwa wamachinga na kununua vyakula kupeleka makwao kwa pesa ndogo wanazozipata pale bongo. Museveni please achilia wengine watawale unaharibu nchi na wananchi sasa watakuchoka. It is true siyo kweli kuwa umeshinda kihalali. Watu wamekuchoka.
ReplyDeleteTunamuombea heri na fanaka kama anapita kwa uhalali.
ReplyDeleteNaona zitapigwa tena Uganda siku moja.
ReplyDeleteHawa viongozi wetu wa Africa kwanini hawapendi kuwaachia watu wengine hali wanajua wameshazeeka? ndo mana watu wanawachoka na kuwatoa madarakani kwa aibu kubwa. Ingependeza sana mzee huyu angeandaa mtu mwingine ktk chama chake agombee nafasi hiyo, hivi kweli hakuna hata mmoja mwenye uwezo kama wake au zaidi ya yeye anayeweza kuiongoza nchi ni yeye tu? Du amakweli kazi ipo, haya na aendelee kucheza rap.
ReplyDeleteHivi nimepitwa, Katiba ya Uganda inamruhusu Rais aendele hadi kifo chake? hana muda? Hivi wanasiasa wan alewa addiction, wanashindwa kabisa kurudi uraiani, wanazowea ukubwa na utukufu hadi anajione yeye peke yake ndio mwenye uwezo. " No body is indespensible" Hivi hasomi alama za nyakati, au wapambe wenye manufaa binafsi wana wa pump hawa wazeee?
ReplyDeleteMhhhh hatari......
Wewe unayesema zimbabwe iliweza kulisha afrika nzima, ni lini hiyo zimbabwe iliilisha bongo? wakati wa miaka hiyo ya themanini tunakula unga wa yanga, hivi ule unga ulikuwa unatoka zimbabwe? usituletee za kitumwatumwa hapa, hivi haiwezekani kuzungumzia jambo bila ya kuchanganya na uongo? au ndiyo another victim of western media, "zimbabwe used to be the bread basket of afrikakakakakakaka" justifying Iain Smith's illegal regime in a decent way. Au ndo wale wanaosema bora wazungu warudi watutawale tena?
ReplyDeleteHata Mubarak alishinda uchaguzi!!!
ReplyDeleteZimbabwe haikuilisha TZ chakula chochote. Labda haujanielewa na pengine sikuongea vizuri ili unielewe. Zimbabwe used to be so well of that it could feed the rest of Africa. Key point there is could. Zimbabwe ilikuwa kama vile South Africa, I lived and worked over there in that time so I know. By the way, I am also a political scholar, so I don't talk or share ideas without having facts. Peace.
ReplyDelete