KIONGOZI wa kundi la Jahazi Modern Taarab, Mfalme Mzee Yussuf alirejea jijini Dar es Salaam leo asubuhi akitokea mapumzikoni Zanzibar na baadae alikwenda Kibaha katika hospital ya Dr Baki kutolewa P.O.P.Baada ya kutolewa P.O.P aliyodumu nayo kwa takriban wiki 4 kufuatia operesheni ya goti, Mzee Yussuf aliruhusiwa kurejea nyumbani kwake ambapo atapata mapumziko ya siku mbili kabla ya kupanda jukwaani Jumapili hii katika onyesho lake la kwanza ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni.
Onyesho lake la pili litakuwa siku ya wapendanao Jumatatu 14/2/2011 katika ukumbi wa Bulyaga Temeke.
Kwa sasa Mzee Yussuf yuko fiti kabisa ila amekuwa kibonge kiasi fulani halafu kaiva ile mbaya si unajua tena mambo ya urojo wa kizanziberi!


Mie sioni kama atakuwa amepona vizuri ,mwezi mmoja autoshi kabisa kwa mfupa kutengemaa,naona ana tamaa ya kujipatia pesa kwenye hii sherehe ya valentine na anaiweka afya yake mashakani...mie najua rehab ya kufanyiwa upasuaji wa mifupa inakuwaje..utasikia mda si mrefu anarudia hali yake ya zamani si ni bora tuu asingefanyiwa huo upasuaji manake aina maana kama atashindwa kurest inanavyotakiwa.
ReplyDelete