Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Johnnie Carson, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt na ujumbe wa maafisa waandamizi wa serikali ya Marekani walikutana na Rais Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine wa Tanzania.

Pamoja na mambo mengine yanayohusu ushirikiano imara kati ya Marekani na Tanzania, Naibu Waziri Carson alijadiliana na viongozi wa Tanzania kuhusu ubia mpya kwa ajili ya ukuaji uchumi, ambao unatokana na Mkakati wa Rais Obama wa kuzisaidia baadhi ya nchi zinazoendelea kukamilisha malengo yao ya kimaendeleo (global development policy).

Mkakati huu ambao Rais Obama aliutangaza katika Mkutano wa Malengo ya Milenia uliofanyika huko New York mwezi Septemba 2010, unalenga kuchochea kasi ya maendeleo endelevu ya uchumi, hususan katika nchi ambazo zimejiwekea mazingira mazuri ya kuwezesha maendeleo.

Marekani inatarajia kuendelea na kuimarika zaidi kwa ubia wake na Tanzania. Marekani ndiye mfadhili mkubwa zaidi wa kiserikali kwa Tanzania ambapo katika mwaka 2010, watu wa Marekani walichangia zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 500 kwa watu wa Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...