MWANDISHI WETU
Dar es Salaam
Mfuko wa Pensheni ya Wafanyakazi wa Mashirika ya Umma (PPF) imepewa tuzo ya kuwa mfano bora miongoni mwa mashirika ya hifadhi ya jamii katika nchi za Afrika Mashariki na Kati katika uimarishaji na uendelezaji wa misingi ya utawala bora.
Tuzo hiyo ilitolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi Thérence Sinunguruza, wakati wa mkutano wa tatu wa Shirikisho la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya Afrika Mashariki na Kati (ECASSA) uliofanyika jijini Bujumbura.
Kwa mujibu wa Meneja Uhusiano wa PPF, Sarah Msika-Kibonde, Sinunguruza alikabidhi cheti maalum kwa mfuko huo wa pensheni wa Tanzania kwa kutambua mchango wake katika kuendeleza misingi ya utawala bora.
Dhana ya mkutano huo ilikuwa ni “Uimarishaji wa hifadhi ya jamii kwa njia ya misingi ya utawala bora’.
Mkutano huo ulihudhuriwa na mawaziri, makatibu wakuu, viongozi wakuu wa mifuko ya hifadhi ya jamii na maafisa waandamizi kutoka nchi wanachama wa ECASSA.
ECASSA inatambua kuwa suala la utawala bora ni muhimu katika kuziwezesha serikali, taasisi za hifadhi ya jamii na mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja katika kuhakikisha kuwa watu wengi zaidi katika nchi wanachama wananufaika na mpango wa hifadhi ya jamii.
Miongoni mwa malengo makuu ya ECASSA ni kuimarisha uwazi, utawala bora na kubadilishana utaalam na utendaji bora katika usimamizi wa hifadhi ya jamii miongoni mwa wanachama wake.
Shirikisho hilo lilianzisha Machi 2007 kutokana na kutambua umuhimu wa hifadhi ya jamii ikiwa ni pamoja na mipango ya afya ya bima na mifuko ya pensheni kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi kwa lengo la kuongeza ubora na ufanisi wa shughuli zake kwa wanachama.
Mwenyekiti wa sasa ECASSA ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Hifadhi ya Jamii Zanzibar Abdulwakhil Hafidh,
“Ni asilimia 20 tu wafanyakazi wote duniani wananufaika na hifadhi ya jamii, na hii lazoima ichukuliwe kama changamoto kubwa kwani hifadhi ya jamii ni haki ya binadamu, na nchi yoyote isiyofuata utaratibu huu inakiuka haki ya msingi ya binadamu,” alisema makamu wa rais wa Burundi kaatika mkutano huo.
PPF iliibuka mshindi wa pili kwa kuwa na taarifa bora zaidi ya fedha kwa mwaka 2009-2010 katika kundi la pensheni ya mifuko ya hifadhi.
Mfuko huo pia umetambuliwa na NBAA kwa kuwasilisha taarifa za fedha katika kiwango cha uhasibu kinachokubalika kimataifa, na hivyo kuongeza imani ya wanachama wake kuhusiana na uwazi katika usimamiaji wa mfuko huo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, tuzo hiyo ina maana kubwa kwa Mfuko huo na inaonyesha jinsi Bodi ya Wadhamini ilivyojidhatiti kuhakikisha kuwa taarifa za fedha zinaendana na viwango vya kimataifa na Sheria inayosimamia Mpango wa Mashirika ya Umma.
PPF inatoa huduma ya hifadhi ya jamii kwa wafanyakazi wote wa mashirika ya umma na kampuni binafsi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...