Picha na 1 na 2. Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Bw. Saimon Mwakifamba(katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Tamasha la Filamu la Mwalimu Nyerere lenye lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo litakalofanyika kwa mara ya kwanza mwezi huu (Februari) 2011 katika viwanja vya Leades Club jijini Dar es salaam.Habari na picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

Shirikisho la Tasnia ya Filamu nchini (TAFF) linatarajia kuendesha tamasha la Filamu za Tanzania la Mwalimu Nyerere ( The Mwalimu Nyerere Film Festival) kwa mara ya kwanza mwezi huu jijini Dar es salaam kwa lengo la kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho hilo Bw.Saimon Mwakifamba amesema lengo la Tamasha hilo ni kukuza soko la kazi za Filamu nchini pamoja na kukuza mahusiano ya kisekta kati ya wasanii wa Tanzania na taasisi za kibiashara za ndani na nje ya nchi.

Ameongeza kuwa licha ya tamasha hilo kuwashirikisha wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu nchini litawashirikisha pia wageni wa tasnia ya Filamu kutoka nje ya Tanzania wakiwemo wageni kutoka Nolywood, Afrika ya kusini na Holywood.

Mbali na hilo amesema kuwa zaidi ya sinema ishirini zilizofanya vizuri ndani na nje ya nchi zitaoneshwa katika Tamasha hilo pamoja na Burudani nyingine zikiwemo ngoma za asili , vichekesho, Muziki wa dansi, Muziki wa Taarabu , Muziki wa kizazi kipya na michezo mbalimbali.

Aidha tamasha hilo kabla ya maonyesho litatanguliwa na mafunzo kwa mada mbalimbali yanayohusu shughuli za filamu na maigizo kutoka kwa wakufunzi waliobobea katika fani, Utunzi , Uongozaji , Uhariri na Ufundishaji.

Tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu ni la kwanza kufanyika nchini litadumu kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 14-19 mwezi Februari 2011 katika Viwanja vya leaders Club jijini Dar es salaam huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. hebu watuambie nani anakuja kutoka Hollywood?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...