Pichani juu na chini ni Sehemu ya majengo ambayo yatakuwa makao makuu ya chuo kikuu huria nchini (OUT) kituo cha Kagera yanayoendelea kufanyiwa ukarabati mkubwa, majengo hayo yalitolewa kwa msaada na mfanyabiashara maarufu nchini anayemiliki kampuni ya Investment solution iliyoko jijini Dar es salaam,Bw. Michael Njumba. Majengo hayo yako maeneo ya Nkyanyi katika manispaa ya Bukoba. Njumba alikuwa amejenga majengo hayo kwa ajili ya huduma za hoteli ya kimataifa. Picha na Audax Mutiganzi, Bukoba


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. safi sana kwa uzalendo,watu kama hawa ndio tunawataka kwa maendeleao ya nchi yetu.ila huyo bwana aitwa IJUMBA.

    ReplyDelete
  2. Huu ndio uzalendo sahihi tunaohitaji kwa watanzania. Mwenye nacho awasaidie wasionacho, sio kwa kuwapa samaki tuu bali kwa kuwafundisha kuvua, ili kesho wavue samaki wao wenyewe. Hongera sana Bwana Ijumba, wewe ni bwenga wa tofauti sana.

    ReplyDelete
  3. Nami nampongeza sana, ameweka hazina yake mahali ambapo haitaoza asilani. OUT wanaweza kumuenzi kwa kuita complex hiyo kwa jina lake.

    ReplyDelete
  4. Nafurahi kuona iki kitu kimetekelezwa nyumbani..! Hope huu ndo mwanzo...

    ReplyDelete
  5. Wewe mdau wa hapo juu acha kubadilisha majina ya watu anaitwa Michael Njumba. Ijumba na Njumba wote ni wahaya. Ila si Ijumba ni Njumba.
    Hongera sana Mzee Michael Njumba, wana Kagera tunathamini mchango wako.Tuko nyuma yako.
    Mdau Stockholm.

    ReplyDelete
  6. Wakola wakola, wakola muno wayoleke ngonzi zawe....!! Tunakushuru Sana Ta Njumba kuleta maendeleo kwetu BK na Tanzania kwa ujumla. Mungu akuzitishie na zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...