Mzozo umezuka nchini Malawi kufuatia mapendekezo kutaka kufikishwa bingeni kuhusu kujamba, kuwa ni kosa.

Waziri wa sheria wa Malawi, George Chaponda amesema muswada huo utakaojadiliwa kuwa sheria ndani ya bunge wiki ijayo, utapiga marufuku kabisa kwa mtu kufanya haja hiyo hadharani. Waziri huyo amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo- kwa maneno yake - "nenda chooni kama unajisikia kujamba".

Hata hivyo mkuu wa wanasheria nchini Malawi Anthony Karanga amesema kufanya haja hiyo hakufikii kuharibu hali ya hewa kiasi cha kuwa kosa la jinai.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema wananchi wa Malawi wanajiuliza mapendekeo ya sheria hiyo, iwapo itapitishwa, itatekelezwaje.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Dawa yake ni kuumwaga kimya kimya mbele ya huyo Waziri wao na halafu unamgeuzia kibao mbele za watu kuwa ni yeye aliyejamba, pambaffff zake.

    Abiola Jr.

    ReplyDelete
  2. hii uwezi kuikataza kinacho takiwa nikuwa na ustraaabu wa jambo lenyewe kwa sababu hii ni sheria ya maumbile uwezi kumkataza mtu kutoa jasho uwezi kumkataza mtu kwenda haja iwe ndogo iwe kubwa au kujampa kwa sababu hayo yote yapo katika sheria ya kimaumbile huu mswada anaotaka kuuwasilisha kwenye bunge sijui wataujadilije ? yaani hakuna matatizo mengine ya kuwakilisha

    ReplyDelete
  3. wamekosa miswada ya maana. Isije ikawa ni agenda ya kuzuga wananchi wahache kujadili mambo ya maana. Shame on them. A poor country should have no time to discuss nonsense especially when the discussion time is paid for by poor citizens' tax through the so called poshos.

    ReplyDelete
  4. Tena watu wengine walikuwa wanauliza kuwa, sasa ukipelekwa mahakamani, ni ushahidi gani utakaotolewa mahakamani kuthibitisha kosa hilo iwapo mtu atakana kosa...Kazi ipo hapo!.

    ReplyDelete
  5. yaani wabunge wamekosa vitu vya kudiscuss baada kudiscuss afrika itaachana vipi na umasikini wanadiscuss mambo ya kujamba

    ReplyDelete
  6. viongozi wa malawi wamekosa la kujadili baada ya kujadili kwa nini wale mashonga waliachiwa na raisi wakati sheria ya nchi inakataza wanajadili mambo ya kipumbavu

    ReplyDelete
  7. huo mswada wenyewe ni ushuzi tu. Hilo haliwezekani kabisaaa ni sawa na kufanya the comedy bungeni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...