Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) akimtwisha, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Madukani, Maria Komba ndoo ya maji yaliyotekwa kutoka kwenye kisima kilichojengwa na Meneja Mradi wa Maji Safi na Afya Bora Ifakara (MSABI), kwa msaada wa TBL. Malulu alifanya juzi ziara ya kukagua visima 10 vya kisasa vilivyojengwa katika shule 10 wilayani Kilombero
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Maji Safi, Afya Bora Ifakara (MSABI), Niklaus Holbro kuhusu kisima cha maji kilichojengwa katika Shule ya Msingi Mtoni, Mjini Ifakara, kwa msaada wa TBL wa sh. milioni 35 . Malulu alifanya ziara Ifakara juzi ya kukagua visima 10 vya kisasa vilivyojengwa katika shule 10
Mjumbe wa Bodi ya Mradi wa Maji Safi, Afya Bora Ifakara (MSABI), Honorati Urassa (kulia) akimshukuru Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Dorris Malulu ) kwa msaada wa sh. milioni 35 zilizotolewa na TBL mwaka jana, kwa Msabi kufanikisha ujenzi wa visima 10 vya kisasa kwa shule 10 Ifakara Wilayani, Kilombero. Malulu alifanya ziara Ifakara juzi ya kukagua visima 10 vya kisasa vilivyojengwa katika shule 10 wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera TBL kwa kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...