Jumla ya warembo 45 ambao wanatarajia kushiriki shindano la kumtafuta Miss Utalii wa Tanzania mwishoni mwa wiki ijayo(5.3.2011) wakiwa katika picha ya pamoja leo jijini Dar es salaam baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari na Rais wa Miss Utalii Tanzania Bw. Gideon Chipungahero.

Mshindi wa shindano hilo anarajia kuondoka na mkataba wa milioni 150 ambao utajumuisha kusomeshwa katika Chuo Kikuu, Gari, fedha za kujikimu na nauli. Shindano hilo litafanyika wilayani Bagamoyo siku ya Jumamosi ijayo.

Warembo hao wanatarajia kushindana kuwania mkataba wa wenye thamani ya shilingi milioni 150 katika shindano la Miss Utalii mwaka huu.

Shindano hilo linatarajia kufanyika wilayani Bagamoyo ambao washiriki kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na wawakilishiriki kutoka vyuo vikuu wanatarajia kuchua vikali kuwania taji hilo.

Kwa mujibu wa Rais wa Miss Utalii Tanzania Gideon Chipungahelo shindano hilo linatarajia kufanyika Jumamosi (5.3.2011) katika Kiromo iliyopo wilayani Bagamoyo.

Alisema kuwa mshindi wa shindano hilo atazawadiwa mkataba utamsaidia kupata elimu ya Chuo Kikuu katika fani ya mawasiliano ya Umma , Gari, nauli na fedha za kujikimu wakati wa masomo yake hayo.

Chipungahelo aliongeza kuwa washiriki wa shindano hilo wanatoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara na wengine wanwakilisha vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo hapa nchini.

Rais wa Miss Utalii Tanzania alisema kuwa, washiriki wote wa fainali za Miss Utalii Tanzania mwaka huu wako katika hali nzuri kiafya na kisaikolojia kwa ajili ya shindano na kufafanua kuwa mbali ya kitita hicho kwa Malkia wa mwaka huu, warembo wengine wataweza kujitwalia mataji yatakayowakilisha hifadhi za taifa 16 zilizo chini ya mamlaka ya hifadhi za Taifa (TANAPA).

Aliongeza kuwa pia, kutakuwa na tuzo zingine toka baadhi ya makampuni na taasisi zilizodhamini shindano hili ili kuyawakilisha katika suala zima la kuutangaza utalii kupitia hifadhi za taifa na utamaduni wa Mtanzania na hivyo kuongeza hamasa zaidi kwa washiriki ambao nao wameonesha kujawa shauku ya kufanya vema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mkubwa,

    Usitusahau Wakubwa wenzio pale watakapokwenda UFUKWENI pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...