Ankal swalama,

Leo usubuhi majira ya saa 2 nilikuwa naelekea town kwa kutumia barabara ya ally Hassan mwinyi road, na baada tu ya st. Peter junction kuna kamchepuo ka kwenda leaders. Kisheria, magari yanayotoka leaders yana option moja tuu ya kwenda direction ya st. Peters junction lakini cha kushangaza – geshi letu la police limemweka traffic police shirikishi pale kusimamia sheria ambaye camera yetu shirikishi imekuta waendesha vyombo vya moto wakivunja sheria mbele ya afande yule kama inavyoonekana kwenye picha!

Mdau wa Lidaz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. kwa kweli madereva wa dar esa laam ni wavunjaji wakubwa wa sheria. hapo huyo askari akimwelekeza utasikia " unanijua mi nani we bwana mdogo sogea nipite ngoja ni mpigie mkuu wako ndio utajua mimi ni nani" keli bongo tambarare........... Mdau karibu asubuhi njia ya chini huku keepleft ya kawe ndio utawajua madereva wa dar !!!!

    ReplyDelete
  2. Barabara za Bongo hazina majina au watu hatujui hiyo mitaa? Hako kamchepuo lazima katakuwa na jina.

    ReplyDelete
  3. inasikitisha na kutia aibu kwa hao traffic police. hiyo moja mimi nilikua noana bora traffic lights ziwe zinazimwa asubuhi na jioni ili traffic police waelekeze magari. i believe hizo taa ziko programmed lakini bado unakuta askari wa usalama barabarani ananza kuelekeza magari na kusababisha foleni sababu hawako proportional wakati wa kuita magari. kama wako wengi wengine wakalinde mitaani mbona wahalifu ni wengi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...