Msanii aliejinyakulia tuzo nyingi za Kili Music Awards 2011,20 Percent

Zoezi la utoaji wa Kili Tanzania Music Awards lilipomalizika hapo juzi pale Diamond Jubilee Hall jijini Dar-es-salaam,jina moja lilibakia katika vinywa na bongo za mashabiki wa muziki na wote waliofuatilia tuzo hizo.Jina hilo sio lingine bali la Abbas Hamisi au maarufu kama kwa jina la kisanii la 20%.

Kijana huyo mzaliwa wa mkoa wa Pwani ambaye unaweza kusema bado ni msanii asiyejulikana sana hususani nje ya mipaka ya Tanzania,aliibuka “Mfalme” kwa kutwaa jumla ya tuzo 5 miongoni mwa vipengele 7 alivyokuwa ameteuliwa katika kuwania tuzo hizo.

Kwa ujumla 20% aliibuka mshindi kama Male Artist of The Year(Msanii Bora wa Kiume), Best Male Singer(Mwimbaji Bora wa Kiume), Best Song Writer of The Year(Mwandishi Bora wa Nyimbo wa Mwaka) na huku kibao chake cha Tamaa Mbaya kikiibuka mshindi katika kipengele cha Best Song of The Year(Wimbo Bora wa Mwaka) na Ya Nini Malumbano kikiibuka mshindi katika Best Afro Pop Song(Wimbo Bora wa Afro Pop).

Kwa bahati mbaya, 20% hakuwepo ukumbini kupokea tuzo zake na badala yake producer wake John Shariza “Man Water” kutoka Combinations Sounds ndiye alikuwa na kazi ya ziada ya kuzibeba tuzo 5 za 20%.

kuona mahojiano yaliyofanywa baina ya 20 % na BongoCelebrity

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Asalaam alaykhum 20%. Napenda sana nyimbo zako kuanzia ile ya kwanza kabisa iliyokutoa nyimbo inaitwa BINTI KIMANZI kisha ukatoa nyimbo inatwa MONEY MONEY ohhhh safi sana kaka real nakubali sana kazi yako ya kutyunga nyimbo pamoja na kuimba. Mola akupe nguvu na afya njema tunednelee kuburudika.

    Chef Issa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...