Meneja Masoko Msaidizi wa Benki ya Exim Anita Goshashy (kulia) na Meneja wa Huduma za WEF wa benki hiyo Felista Simba (katikati) wakibadilishana mawazo na baadhi ya washiriki wa warsha na maonyesho ya siku moja kwa Wajasiriamali Wanawake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki

Baadhi ya washiriki wa warsha na maonyesho ya siku moja kwa Wajasiriamali Wanawake yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Dar es Salaam wakifuatilia mada kutoka kwa muwezeshaji Jacqueline Maleko wa Wizara ya Viwanda na Biashara (hayupo pichani). Benki ya Exim kama moja ya benki zinazowezesha Wajasiriamali ilialikwa kutoa elimu ya akaunti yake ya Tumaini ambayo ni maalumu kwa Wajasiriamali Wanawake.

BENKI ya Exim Tanzania imedhamiria kuinua kipato cha Wajasiriamali wadogo ambapo imepanua wigo wa huduma zake za kifedha kwa kufungua akaunti ya Tumaini maalumu kwa ajili ya Wajasiriamali Wanawake.

Akizungumza katika maonyesho maalumu ya wajasiriamali wanawake yaliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Masoko Msaidizi wa benki hiyo Anita Goshashy alisema hatua hiyo ni ya kutambua nafasi ya wanawake katika uzalishaji.

Alisema wanawake wa dunia ya leo wanachukua nafasi kubwa katika maamuzi ya matumizi ya familia, kuweka akiba na uwekezaji wa malengo ya muda mrefu ndani ya familia hivyo akaunti hiyo imelenga kuwasaidia wahusika kumudu majukumu hayo na mengine ndani ya jamii.

“Tuna huduma nyingi za kifedha za kuwawezesha wajasiriamali lakini tulikaa na kuona haja ya kuwa na kitu cha kipekee kwa wanawake na kuja na Akaunti ya Tumaini maalumu kwa ajili yao,” alisema Goshashy.

Alifafanua kuwa akaunti hiyo imegawanywa katika makundi mawili ya akaunti kwa ajili ya matumizi ya kila siku na nyingine ni kwa ajili ya akiba kwa matumizi maalumu kama ada za shule, biashara, gharama za afya na nyinginezo ikiwa ni pamoja na kumwezesha mteja husika kupata mkopo kupitia akiba yake ndani ya akaunti hiyo.

Goshashy alisema akaunti hiyo ina kiwango kikubwa cha riba tofauti na akaunti nyingine hivyo kuwezesha akaunti husika kukua haraka.

“Tumedhamiria kuwawezesha wanawake, akaunti hii itamuwezesha mwanamke kumudu mahitaji ya kila siku lakini pia itamuwezesha kuwekeza katika mipango ya muda mrefu ya familia na jamii yake,” alisema.

Maonyesho hayo yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania yalitanguliwa na semina kwa wajasiriamali husika ambapo muwezeshaji Jacqueline Maleko kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara aliwataka wanawake kuchangamkia fursa za uwezeshaji zinazotolewa na wadau mbalimbali kwani ndio njia pekee ya kujikomboa.

Alisema wanawake wamekuwa wakitumika kuinua sekta nyingi nchini bila wao kupata fursa ya kutosha kuinuka hivyo aliwataka kubadili mtazamo na kuangalia njia zinazoweza kuwakomboa kwani jamii hiyo bado ipo nyuma katika mambo mengi.

“Tumekuwa tukiwekeza nguvu nyingi katika maendeleo mbalimbali nchini lakini tumekuwa hatupati nafasi ya kutosha kujiinua hivyo tunapaswa kubadilika na kuwekeza zaidi katika njia tunazoona zitatusaidia kuinuka kwa haraka,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ndg. Michuzi, samahani natoka nje ya mada kidogo. Kufuatia janga la tetemeko huko Japan, kuna jumuia ya watanzania nchini Japan (Tanzanite Society Japan) imetoa habari katika website yao, kama ukiona inafaa naomba uirushe mtandaoni ili watu waweze kujua yayoendelea juu ya ndugu zao waliopo huko Japan kwa kuuliza kupitia anuani iliyotolewa. Website ni http://www.tanzanitesociety.jp/announcement/show/11/

    Naomba kuwakilisha.
    Asante
    MDAU

    ReplyDelete
  2. Babu kubwa Anitha naona unawakilisha watoto wa Jitegemee kwa Masawe. Safi sana hakikisha wajasirimali wanasaidiwa vilivyo nakuaminia kuchakachua pia kupo. Mdau wa Texas!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...