Kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha na mkuu wa wilaya ya Arusha Mh. Raymond Mushi (katikati)akizindua huduma ya mikopo kwa wakulima wadogo kwa kupampu maji kwa ajili ya kumwagilia bustani za mboga mboga.

Picha na habari na Woinde Shizza, Arusha

BENKI ya NMB imezindua rasmi mpango wa kukopesha wakulima wadogo wa mbogamboga na bustani,kuwawezesha kupata pembejeo, dawa za kuulia wadudu na mbolea kwa bei nafuu.

Huduma hiyo itawasaidia wakulima hao kutotegemea mvua pekee katika uzalishaji wa mazao hayo katika kipindi cha mwaka mzima.

Mkuu wa kitengo cha kilimo,NMB ,Robert Pascal aliyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma ya mikopo na pembejeo kwa wakulima wadogo iliyofanyika katika eneo la Olasiti,mkoani Arusha,na kuongeza kuwa uzinduzi huo ni wa kwanza mkoani Arusha na utafuatiwa na mikoa mingine.

Alisema tangu mpango huo umeanza mwaka 2008 ,kiasi cha shilingi bilioni 13.2 kimetolewa kwa wauzaji pembeje wa 966 katika wilaya 38 nchini ili ziwafikie wakulima .

Alisema kuwa NMB imewakopesha wakulima wa mazao mbalimbali wa Miwa eneo la Turiani na kilombero ,Chai wakulima wa Lushoto na wakulima wa Ngano waliopo mkoa wa Arusha,Ambapo kiasi cha shilingi bilion 54 zimetumika hadi mwaka 2010.

Pascal alisema, mikopo hiyo italipwa na mkulima kwa riba nafuu katika kipindi cha miezi 10 tangu mkopo ulipochukuliwa,hivyo kilimo hicho cha mkulima mdogo kinatajaria kuongeza tija na mazao mengi kuongezeka.

Kwa upande wa mkuu wa wilaya ya Arusha ,Raymond Mushi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ,pamoja na kuipongeza NMB kwa kuona umuhimu wa kuwekeza katika kilimo kwa kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo,alisema hiyo ni fulsa muhimu kwa wakulima hao kuongeza uzalishaji na pato la mkoa kwa ujumla.

''Hii ni fulsa muhimu na kubwa kwa mkoa wetu na sina shaka wakazi wa Arusha wataitumia kikamilifu kuongeza uzalishaji katika kilimo ,ukizingatia mkoa wetu umekuwa wa kwanza kuzinduliwa kwa huduma hiyo,nawatia shime NMB kwa huduma yao ya kujali mapinduzi ya kilimo cha kijana''alisema Mushi

Alisema kuwa changamoto kubwa inalowakabili wakulima kushindwa kuleta mapinduzi ya kilimo cha kijani nchini ni kutotilia mahanani kilimo cha umwagiliaji na matumizi hafifu ya rasilimali maji,ambayo ni rasilimali ya msingi katika kilimo chenye tija husushani katika kipindi hiki chenye mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mushi ametoa rai kwa taasisi nyingine za kifedha kuona umuhimu wa kujikita na kuwekeza kwenye kilimo kwanza kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua uchumi wa mtu mmoja na kuongeza pato la taifa kwa ujumla


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...