huko Urban quarters Tabora jioni hii..
Dada Magreth Mutalemwa kabla ya kutoa kikombe cha dozi
Dada akiomba dua kabla ya kumpatia mgonjwa kikombe
Hapa hadi kieleweke...
Wakubwa kwa wadogo wamejitokeza kwa Dada
Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora, akijiandaa kwenda kutoa kikombe leo
Umati nyumbani kwa dada leo
Umati ukisubiri huduma
Ulinzi waimarishwa kwa dada
Diwani Zinduna Kambangwa akitoa ushuhuda kwa OCD wa wilaya ya Tabora nyumbani kwa DADA eneo la uzunguni au urban quarter muda mfupi uliopita.
Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora mjini, amejitokeza na kudai alioteshwa kutibu watu na Bikira Maria, mpaka sasa OCD yupo hapo kwa dada na amemwambia mdau wa libeneke la kerongingi, Mkala Fundikira, kuwa yeye alishapata kikombe toka kwa dada na amejitapa hatoondoka pahala hapo mpaka askari zaidi watakapowasili kuongeza ulinzi.
Watu kadhaa wameonesha imani na dawa ya dada na kusema wana nafuu tangu wanywe dawa yake ambayo bado haijafahamika chanzo ama mchanganyiko wake. Ila bei ni ile ile ya Babu yaani sh. 500/- a.k.a Jero.
foleni ili kupata kikombe cha DADA
Baada ya Babu Loliondo, Mangi Tarakea na Dogo wa Mbeya, mtu mwingine ameibuka safari hii toka mkoani Tabora, akito kikombe anachodai kinatibu maradhi sugu, na kuvutia umati mkubwa wa watu wa mji huo mkongwe.
Dada Magreth Mutalemwa mkazi wa Urban Quarter Uzunguni, Tabora mjini, amejitokeza na kudai alioteshwa kutibu watu na Bikira Maria, mpaka sasa OCD yupo hapo kwa dada na amemwambia mdau wa libeneke la kerongingi, Mkala Fundikira, kuwa yeye alishapata kikombe toka kwa dada na amejitapa hatoondoka pahala hapo mpaka askari zaidi watakapowasili kuongeza ulinzi.
Watu kadhaa wameonesha imani na dawa ya dada na kusema wana nafuu tangu wanywe dawa yake ambayo bado haijafahamika chanzo ama mchanganyiko wake. Ila bei ni ile ile ya Babu yaani sh. 500/- a.k.a Jero.
Kamati ya ulinzi na usalama itakaa muda mfupi kujipanga na mfumuko wa watu watakaokuja kufuta huduma ya dada Magreth Mutalemwa. Mkuu wa mkoa ndio huyo anaingia sasa na tunasubiri kauli yake juu ya hili. Habari zaidi zitaendelea kuwajia wapendwa wadau na ukitaka zaidi nenda http://www.keronyingi.blogspot.com/
NGOJEENI SASA AJE MTU ASEME KAOTESHWA NA NYERERE SERIKALI IMPE BILLION ZA TANZANIA 500 BASI ZITATOLEWA WATANZANIA TUNA MATATIZO SI MCHEZO. HUYO ATAYESEMA KAOTESHWA NA NYERERE CHADEMA WATAMGOMBANIA KWELI KWA FURAHA LOL.
ReplyDeleteMIE NA WASIWASI NA BABU AMBILILE A.K.A WA LOLIONDO ANAWEZA KUWA WENGI HII DAWA WALIKUWA NAYO SEMA KUNA MTU KAMSHAURI ATANGAZIE WATENGENEZE PESA HUYU BABU KAVUNJA SHERIA ZA KUTANGAZIA DAWA NDOMANA WENZAKE WAMEONA NAO WATANGAZIE AU MNAONAJE WADAU?????? MZ.
Nataka waibuke kila Mkoa wa Tz. ili wapunguze Foleni Kwa BABU wa Loliondo!ili tunaokwenda kule tuwe wachache!! tehe tehe tehe!
ReplyDeletejohn mashaka na mjengwa chambueni hili nalo?
ReplyDeleteSwali, jee hii mijihela wanayoikusanya inakatwa kodi?
ReplyDeletesi mchezo dozi kila kona,mpaka akina ras makunja nao wanajifanya wanalinda kumbe wapo ktk foleni ya kupata kikombe
ReplyDeleteMashaka na Mjengwa wamepania Babu, lakini hawawezi kushambulia huyu mama na wengineo kwa kuwa wao ni wapingaji wa mambo ya Mungu ya kweli.
ReplyDeleteKweli tunaomba wote wanaompinga babu wajiunge na huyu mama au jafari wa mbeya au yule wa kule Tarakea.
Sisi watuachie mchungaji wetu wa Loliondo.
Sijawahi kusikia shehe Yahaya akipingwa ijapokuwa huwa anafundisha uchawi live!
Sasa simmeanzisha ligi kila dhehebu litaoteshwa. Mliomkataa Mchungaji nendeni kwa Bikira maria
Ujinga wa WaTanzania,umasikini wa kufikiri ni kitu kibaya sana,uupuzi mtu!
ReplyDeleteNdoto ya Mchana,Sweden
Anaon wa Shehe Yahya, hujawahi kusikia akipingwa, kwani uk wapi? Huyo naye ni mjasilia mali tu kama wengine, na watu wa dini wamekuwa wakimpinga sana tu. Hata hivyo , yeye huhusisha tiba zake na Majini na sio Mungu, kama hawa wajasilia mali wa sasa!
ReplyDeleteWatanzania bado sana kwakweli inasikitisha watu wanadanganywa kiasi hiki.
ReplyDeleteHATA SERIKALI INASHINDWA KUDHIBITI MAMBO YA KIPUUZI KAMA HAYA.
Hivi hawa walikuwa wapi muda wote? Walikuwa wanangoja yule wa Arusha aanze?
ReplyDeleteHuyu ni bijampola, kuweni macho
ReplyDeleteKama kweli mti unaotumiwa na Babu wa Loliondo ni Carissa Spinarum basi tafiti na matumizi yake dunia nzima hizi hapa na wala babu si mtu wa kwanza kuutumia huu mmea kutibu watu. Vilevile si kweli kuwa alioteshwa na Mungu wala si kuwa ili ufanye kazi ni lazima ufuate masharti ya babu na hauhitaji imani ili kufanya kazi na zaidi ni kuwa si lazima unywe kwa babu wala kutolewa Loliondo pekee au babu pekee. Wewe mwenyewe unaweza utumia mti huo kwa shida hizo kama zinavyoonesha kwenye tafiti za kimataifa kuhusu mmea huo.
ReplyDeleteInavyoonekana ni kuwa babu alipewa ujuzi huu wa huo mti na watu fulani hapo arusha ambao wamekuwa wakiutumia kama dawa akafanya utafiti wake na kugundua kuwa unakubalika sehemu mbalimbali hapa dunianai kuwa ni dawa na kwa kuwa wabongo ni mambumbumbu akijifanya kuwa kaoteshwa basi wote watafuata foleni na ili kujihakikishia monopoly na kipatoa akatoa masharti kuwa ni lazima yeye akupe nani lazima iwe loliondo na ni lazima ufuate foleni na kadhalika na kadhalika. Hiyo yote ni sanaa tupu, yaani kwa ufupi ni utapeli.
Nikirudi kwenye mmea wenyewe na lengo hasa la mimi kukaa mbele ya kompyuta yangu na kuandika haya ni kuwa mti huu umekuwa ukitumika duniani kote hata Tanzania kama tiba ya asili ya magonjwa yaliyotajwa na mengine, sema watu wengi hawalijui suala hili nami pia sikujua hasa jina la mti anaotumia babu kisayansi mpaka taarifa ya serikali kuhusu uchunguzi wa dawa ya babu ulipotoka kuwa mmea huo unajulikana kama Carissa Spinarum.
Kwa ufupi ninawapatieni links za tafiti na matumizi mmea huo Carissa Spinarum kamaifuatavyo:
http://www.stuartxchange.org/Caranda.html
http://www.ajol.info/index.php/tjpr/article/viewFile/44519/28024
http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/19775072
Nyingine zitafuata baadaye, hii ni kutaka tu kuweka mambo sawa kuhusu madai ya babu kutokewa na Mungu na kupewa masharti ya jinsi ya kutumia au kugawa dawa hiyo.
Kwa ufupi ni kuwa maelezo ya babu ni uongo mtupu, isipokuwa mmea huu unakubaliwa kuwa unatibu magonjwa mbalimbali duniani kote na umekuwa ukitumika siku zote na hata Tanzaniahivyo si kitu kigeni wala cha ajabu kama inavyodaiwa.
This is another DECI, or a so called bomb yet to explode....
ReplyDeleteKuna siku watu watakunywa sumu. Utasikia wamekufa maelfu ya watu baada ya kunywa hizo concoctions za ajabu.
ReplyDeleteJamani Jamani, hii sasa imekuwa imezidi, Unajua watanzania wana tabia ya kuiga sana, wengi sio wabunifu au waanzilishi wa ni watu wa kucopy and paste)Wanasubiri mtu aanze kitu/jambo fulani na wao ndio waibukie huko. Kwa mfano, mtu akianza kuuza vitumbua hapa kesho anaibuka mwingine tena na vitumbua vya aina hiyo hiyo mahali pale pale. Hii iko kila mahali na sasa ndio inajitokeza kwenye haya mambo ya NDOTO ZA VIKOMBE zinazokuja kwa stahili ile ile ya kuoteshwa au kukutana na Mungu, roho mtakatifu au malaika.
ReplyDeleteLakini kinachonistua na kunishangaza ni jinsi watu wanavyoweza kuwaamini hawa watu kirahisi namna hiyo na kuvutwa kwa kasi ya ajabu.Hivi kila anayeota kuhusu kikombe sasa basi anafaa kusikilizwa na kufuatwa kwa kasi ya ajabu??? Hivi wengine hawawezi kuwa matapeli au mapandikizi wenye nia ya kujipatia fedha kwa wateja wapya au kugawana watu walioenda SAMUNGE kwa babu?? Jamani ni wangapi tumeota ndoto nzuri na za kuvutia kuhusu sisi wenyewe, nchi hii na watu wake? Je wote hawa wakiamua ku-implement ndoto zao itakuwaje? Pamoja na hoja kwamba kwamba huduma za afya ziko chini na watu wamekata tamaa lakini sasa imezidi. Je kila anayeota anaweza kuwa ni mbadala wa huduma duni za afya nchini???? Na bahati mbaya katika hili hatujaona wazee wala watoto (angalia picha za maandamano ya mbeya kumuunga mkono babu dogo)
Ningependa kushauri kwamba imefika mahali watanzania tujenge utamaduni wa kutoa majibu magumu na sahihi kwenye maswali magumu. Maswali ya uponyaji wa vikombe vyote hivi yanahitaji majibu sahihi kwa maana kwamba ndugu X alikuwa anaumwa au anaumwa ugonjwa Y kwa muda Z, na imethibitiswhwa hivyo na vituo sahihi vya afya vinavyotambulika. Na baada ya kikombe cha babu, babu dogo, mangi au dada siku kadhaa zilizopita ameenda kupima tena (control check up) na kugundulika kwamba ugonjwa Y UEMTOWEKA. Then hapo, tunaweza kuongea mengine.
Nina imani, huu uyoga wa ndoto za vikombe utaendelea maanza watz ni mabingwa wa kucopy and paste na kuna uwezekano wa matapeli kujipenyeza huko huko as long as kuna 500/=. Mia tano mara hata watu kumi kwa siku ni shilingi 5000/= inaweza kuwa bisahara nzuri kwa wajanja. Dadisi.
Naomba kuwakilisha ankali.
Common mwananchi
mbona kila mtoa dawa anatumia kikombe tuuuuuuuu,kazi kweli kweli,nashindwa nicoment nini jamani loh,yanakuwaje mambo haya?
ReplyDeleteNimesikia kuna mkakati wa waganga wa kienyeji wote pamoja na wachawi waliokubaliana wote wajitokeze nchi nzima kudai kuwa wameoteshwa kutoa tiba.
ReplyDeleteNdio maana wote wanaigiza mtindo wa kutumia kikombe wakati waganga wote walikuwa wanatoa dozi mbali mbali. Na wote wamekubaliana watoze sh. 500 tu kumuigiza mchungaji.
Lengo lao ni kuishinikiza serikali iwafungie wote wanaotoa tiba ikiwemo mchungaji kwa kuwa mchungaji ameharibu soko lao.
Kawaida waganga walikuwa wanaomba kuku, mbuzi na walikuwa wanatoza pesa nyingi lakini ili kupambana na mchungaji wameamua kutoza sh. 500
For real hii imekuwa kama uganga sasa. Kila mtu anakuja na dawa yake kila siku! Na Watanzania kabisaa na akili zenu mnakubali bora mwende, huku mkiwa hamna ushahidi wala nini. Eh, jamani watu,mmefanya imani kuwa kama biashara. Ukioteshwa tu, hata ndoto ya uongo sasa utatengeneza dawa yako. Serikali, please do something about this, au kama vipi, hawa nao wasajiliwe kama waganga wanavyosajiliwa. Si imani vilevile?
ReplyDeleteKWELI THIS IS A HERD MENTALITY.. YAANI WAMEKOSA KAZI YA KUFANYA AU NI DALILI ZA KUCHOKA NA MAISHA. KWELI ITS SAD.. WANATAFUTA Dawa lakini reality wamechoka na maisha. Kila siku promises lakini hamna lolote
ReplyDeletehahahaha watu pipo.Its a simple issue kujua maji yanajitenga na mafuta.Hao wanaosema wameoteshwa naomba niwasahihishe WAMEOTA.Ni kawaida mtu kuota jambo analowaza,tena especialy hawa wenye kusali na kuabudu.So tutegemeee wengi kusema wameoteshwa kumbe Wameota.Nachoweza kusema Ni Mchungaji Ambilikile alioteshwa kitambo sana,hakukurupuka na kuanza kugawa vikombe,ilimchukua mda mpaka akaoteshwa tena na ndipo alipoanza kutoa dozi tena kwa yule alielekezwa.Hawa wengine,wameota tu,watoe dawa tu,kwa watu tuu.?
ReplyDeleteJamani Mungu hataniwi wala umaarufu si mpaka ugawe vikombe,kama huyu mama si aseme kwanini anachaji jero?anatumia kikombe?Baada ya Ambilikile.
We have a lot to see jamani
Mdau
ha haa haaaaaaaaaaaa, zecomedy si kina masanja peke yao tehee tehee wa rombo nae akaja na kikombe tene na kuiagiza serikali itengeneze miundo mbinu huko tarakea watz bwana raha tuuu!!!! sa hizi kila mtu na kikombe chake cha ndoto mie aah hata watokee 20,000 kikombe cha babu loliondo ndio original wengineo wote WANACHAKACHUA, HALAFU SIO WABUNIFU kila mtu kikombe loo hata haya hawana,uso umeumbwa na haya jamani,tuoneeni huruma binadamu wenzenu na hizo ndoto zenu
ReplyDeleteNafikiri kimsingi polisi wanakosa haki kisheria kuwatia watu hao hatiani, kwa kuwa hawavunji sheria yeyote ya nchi, polisi huwashauri watu hao waombe kibali cha kugawa dozi zao. Na serikali ikipima dawa hizo na kuona hazina madhara kwa matumizi ya binadadamu nao wanalkosa nguvu ya kuchukua hatua yeyote!
ReplyDelete