Habari Ankal na Wadau wa Globu ya Jamii
Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu wananchi wa maeneo ya Kibanda, Kigamboni, na maeneo ya jirani na Zoo na Dar es Salaam nzima kwa Ujumla, kuwa taarifa za kutoroka kwa kati ya Simba wetu kwenye Zoo sio za kweli.
Simba wetu wote wako salama pamoja na Wanyama wengine wote. Simba alie patikana maeneo ya Mbagala na huyo mwingine anaesemekana kuepo maeneo ya huko hatoki kwenye Zoo yetu. Kuhusisha Dar es salaam Zoo na wanyama hao ni Uzushi na Tetesi tu za mtaani. Si za kweli asilani.
Karibuni Sana Dar es Salaam Zoo
Akhsanteni Sana.
Mr. Salim Hassan
Marketing manager
Dar Es Salaam Zoo
+255 784 524285

Bwana Salimu tueleze kwa kina, je kuna ukaguzi/inventory uliofanywa kwenye Zoo yenu na idara ya maliasili kabla na baada ya tukio hili kubainisha idadi halisi ya simba mliyonayo kabla na baada? Na kama ilifanyika je matokeo yalikuwaje, na Je idara ya maliasili huwa inafanya ukaguzi ma mara kwa mara wa inventory yenu halisi na suala zima la utunzaji wenu wa wanyama hao? Je ripoti hizo unaweza kutuonyesha sisi wadau maana si siri kwani mnatuhudumia sisi wananchi.
ReplyDeleteAlex Bura, Dar
Ebu waacheni hao kina simba wkakae kwa uhuru huko serengeti ebo!
ReplyDeleteJAMAANI MBONA VICHEKESHO,MAANAKE NIMECHEKA MPAKAA, WANANCHI WANADAI SIMBA WENU, NANYI MWASEMA SIMBA SI WENU SASA HAO SIMBA HUKO MBAGARA WATOKA WAPI? MBONA SHUGHULI SIMBA KUJA KWENYE MAKAZI YA WATU, JAAMANI NA HUKO MBAGARA, KAZI KWELI KWELI.
ReplyDeleteWanyama wanamazingira yao.... Hata kama ni zoo izingatie hilo.......
ReplyDeleteUkaguzi unafanyika na Serikali kupitia mamlaka Husika, na Pia sisi wenyewe tuna utaratibu wa kukagua mazingira,na vitu vyote vinavyo tuhusu!
ReplyDeleteUtaratibu wote unafuatwa kuendesha Zoo yetu!