Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Nouakchott tayari kushiriki katika kikao maalumu kinachojadili mchakato wa amani ya Ivory Coast. Rais Kikwete yupo katika kamati maalum ya marais wa nchi za Umoja wa Afrika (A.U) yenye lengo la kuleta suluhu ya mgogoro wa kisiasa nchini Ivory Coast.Marais wengine waliopo katika kamati hiyo ni Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini,Rais Blaise Compaore wa Burkina Fasso, Rais Idriss Deby wa Chad na Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Mohamed Ould abdel Aziz wa Mauritania wakikagua gwaride la mapokezi lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nouakchott tayari kushiriki katika mazungumzo ya amani ya Ivory Coast.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini na Rais Balise Compaore wa Burkina Fasso wakiingia katika kikao maalum cha kamati ya Umoja wa Afrika (AU) yenye lengo la kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast.Kikao hicho kilifanyika katika mji mkuu wa Mauritania Nouakchott. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...