Mwenyekiti wa kamati ya mashirika ya umma na hesabu za serikali (POAC) Mh. Zitto Kabwe akitazama madini ya chuma huko mchuchuma wilayani Ludewa. Madini hayo yapo nje nje kama yanavyoonekana hapa

Mwenyekiti wa kamati ya bunge hesabu za mashirika ya umma Zitto Kabwe na makamu wake Deo Filikunjombe wakitoka kutazama madini ya mchuchuma eneo la Mkomang'ombe Ludewa
Waheshimiwa wakiwa Mchuchuma
Juu na chini ni kamati ya bunge, viongozi wa NDC na waandishi katika mgodi wa madini ya mchuchuma Ludewa
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu ya mashirika ya umma , Zitto Kabwe (wa pli kulia) akiwa na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), Chrisant Mzindakaya (mwenye pama)wakisikiliza maelezo kuhusiana na utafiti wa chuma katika mgodi wa Turawaka, wakazi kamati hiyo ilipotembelea, eneo hilo Ludewa mkoani Iringa.
Picha na Francis Godwin

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Haya ndo mambo inabidi tubadili kwenye Katiba mpya. Kamati ya Bunge yatembelea mgodi ambao mwenyekiti wa bodi ya mgodi ni Mbunge mwenzao!! Maajabu haya! Nani atamfunga paka kengele!

    ReplyDelete
  2. Nadhani pengine mchanganyiko huu waweza kuzaa matunda fulani japo yaweza kuwa ni kwa muda mrefu. Lakini picha za utajiri huu ni aibu kuona miaka yote hii hautuutumi na bado twalia njaa. Tuiombee kamati hii iwajibike japo chuma hiki kitutoe basi!!!!

    Mbunju

    ReplyDelete
  3. Jamani Tanzania Mungu ametupa NEEMA Kubwa namna hii bado tunahangaika na Umaskini?

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni economic system mbovu. Ujamaa utaendelea kutueletea umaskini mpaka siku tutakapoutupa kama nyoka na kuukumbati ubepari. Haya madini yangekuwepo kwenye nchi za kibepari nchi ingeendelea vibaya mno.

    ReplyDelete
  5. Anonymus Tue Mar 08, 06:45:00 pm2011 - unayo sema ni correct kabisa kwamba Mungu ametupa NEEMA kubwa -na bado tunahangaika - ndiyo na wengi watakwambia ni mafisadi na mapapa's hao wanatu malizia, lakine hii sio ukweli - but this is the resposibility of serakali yetu ambaye baado ni mchanga na hawana budi yakuendeleza inchii yetu...kwa mfano - tangu miaka 70 or 80 cheki accidents on our roads - sijawahi kuona even one government official to stand up and say - enough is enough -but hao baado wanaendelea ku travel in big convoys and let poor people fend for them selves on the roads i have not seen a reporter/blogger or wananchis take action against these officials...but it is very easy to put a SPIN on wafisadi and corruption -and it is true it plays a role but officials in the ministry should be fired for every big accidents on transport buses....does any one agree with me?

    ReplyDelete
  6. ...We Anony wa kwanza unaishi wapi weye?, Mzindakaya (Mwenyekiti wa Bodi ya NDC)si mbunge. Alishastaafu ubunge.

    ReplyDelete
  7. Mikausho MikaliMarch 09, 2011

    hayo ni makaa ya mawe si chuma

    ReplyDelete
  8. Ludewa ina neema zote mbili za makaa ya mawe-Mkomang'ombe na chuma katika maeneo ya Liganga.

    Na makaa ya mawe yamewekwa na mungu ili yatumike kufua chuma. Ni muujiza kwakweli huwezi amini iweje viwe pamoja.

    Chuma iliyopo Ludewa-Liganga ni chuma ngumu sana ila nyepesi inayofaa kutengenezea bodi za ndege. Mtaalam mmoja aelezee kwa urefu chuma hiyo ili watu watoe machozi utamu na uzuri wa madini hayo ya hapo Ludewa. Hiyo chuma inapatikana Brazil na ya huko Brazil haifikii ukubwa na ubora wa hii ya Ludewa

    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  9. ndugu yangu uliyeutukuza ubepari hapo juu, issue sio ujamaa ujamaa. Kama ubepari ungekua suluhu Congo ya Mobutu na Kabila ingekua tajiri sana leo hii. Ingawa wao ni masikini kuliko hata Tanzania ya kijamaa pamoja utajiri wao wa rasilimali. Kikubwa ni sera safi na watu walio na uzalendo, ambao sidhani kama wewe binafsi unao!

    ReplyDelete
  10. Mdau wa March 9, 11:41
    Congo hawafuati Free Market Capitalism. Capitalism na Freedom vinaendana bega kwa bega. Mobutu alikuwa ame side na Western powers kwenye cold war but hakufuata nyayo za ubepari kama economic system ya nchi yake.

    Angalia mfano wa nchi kama Singapore, Korea ya Kusini, Hong Kong, na Taiwan jinsi zilivyoendelea kwa ajili ya ubepari.

    Watanzania kila siku tunalalamika hali ngumu ya maisha bila kujua solution ya matatizo yetu. But nashangaa tumeshindwa kugundua kuwa tatizo ni Ujamaa. Ujamaa utaendelea kutufanya kuwa maskini mpaka siku ambayo tutaukumbatia ubepari kama Wachina wanavyofanya sasa hivi.

    Free Market Capitalism is the only path to prosperity.

    Long Live Free Market Capitalism!

    ReplyDelete
  11. mnaongelea utajiri na neema ya hiki chuma tulichojaaliwa,lakini mkumbuke kwamba mchina kashakabidhiwa achimbe hiko chuma kwa miaka mitano(5)baada ya hapo sidhani kama kutabaki kitu.

    ReplyDelete
  12. "..Angalia mfano wa nchi kama Singapore, Korea ya Kusini, Hong Kong, na Taiwan jinsi zilivyoendelea kwa ajili ya ubepari.."

    Duuh!?

    ReplyDelete
  13. tunadhani misaada tunayopewa ya kujengewa barabara inatoka bure. naamini mwenye akili hatasfiriwi. kama mchina au mjapani unadhani watatoa misaada bure bure???watu wameibinafisa nchi ziku nyingi tu lakini hatuna upeo wakujua. tutazungumza siku mbili tunakaa kimya hatuna hata uchungu. Sijui wanaokaa maeneo yanayozunguka madini hayo sijui hali zao ziko wapi. Watanzania tuwe na uchungu na kwakujua kuna kizazi kinafuata kinahitaji neemea kama hizi. tuache kusaini mikataba mibovu kwakujinufasha mtu au kikundi fulani. Shibe ya muda mfupi isitufanye tujawa na njaa ya miaka na miaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...