
-BWANA ALI SHARIFF ni mzaliwa wa mwaka 1898 na alikuwa mshauri wa BABA wa taifa Malim Nyerere na Ali hassan Mwinyi baada ya kustaafu kwenye mwaka 1980.
- Mshirazi wa kwanza, Sheikh Ameir Tajo, aliteuliwa kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria akifuatiwa na mwenzake, Sheikh Ali Shariff Mussa, aliyeteuliwa mwaka 1948 na mfalme Sayyed Khalifa bin Harub Al-Busaidi.
-kwenye 1930s hadi 1950s alichaguliwa kuwa ni MBPE Member of British Empire Perliamnent.( hizi habari zote zipo hadi leo Commonwealth na Lancaster house Uingereza)
-muasisi wa Zanzibar and Pemba Peoples Party (ZPPP) mwaka 1959. Baada ya kuanza mgogoro na fitna za watu na Afro Shirazi Party.
- ni mwananchi aliyesimamia ukoloni wa kizungu kuisha na uuzaji wa utumwa east Africa, katika lancasta house uengereza.
-alipofuka macho 1972 baada ya kupotea mdogo wake Bwana Othman shariff.
-alistaafu mwaka 1980 sababu ya uzee lakini Baba wa Taifa Malim Nyerere alikuwa akimtembelea kila baada ya muda pamoja na Bwana Ali Hasan Mwinyi, na Mzee ABoud Jumbe.
-Bwana Ali Hassan Mwinyi ndie aliekuwa mtu wake wa mwisho kumtembelea na 1987 kwa miezi michache ndio mzee kufariki.
-aliowa wake nane katika maisha yake lakini alizaa na wake watatu tu.
-azimio lake lilikuwa ni kuitumikia Tanzania na kuboresha elimu ,afya ,na maisha bora kwa kila mtanzania baada ya kuwashinda wazungu katika mahkama yao huko uengereza na kuondoa ubaguzi wa makabila na utumwa ndio kisa cha afro shirazi kuanza ilikuwa ni mashirazi kushirikiana na wafrika tofauti ili kuimarisha Tanzania.
-alifariki dunia tarehe 05/03/1988 kukamilisha miaka 90 umri wake huko mji wa Wete, Pemba, na Skuli ya college of London inamsoma katika vitabu vyake kama ni mmoja katika kiongozi aliokuwa na subra na busara mpaka wazungu wakampa jina la utani (the owner of Pemba island) sababu alichokuwa akisema wapemba wengi wakimsikia ndio yeye sababu ya kutoa viti vitatu na kushinda afro shirazi enzi ya Bwana Abeid Karume.
-leo tarehe 06/03/1988 ndio siku aliozikwa saa nne asubuhi mjini Pandani alikozaliwa. Bwana huyu kwa sasa kuna kitabu kipya kimetunga na Proffessor Michael Kutoka university of Los Angeles, Yeye ni dean wa hicho chuo huko Marekani na amezungumzia maisha ya Marehemu Bwana Ali na Busara za kisiasa wakati ilipokuwa Tanganyika kuwa Tanzania na kwa sasa anatengeneza museum( makumbusho ndogo ya Zanzibar na Tanzania) kwenye hiyo University ili kuwaonesha wamarekani kama Tanzania ilikuwa na viongozi wenye busara na hikma mpaka kupapatuana na ukoloni.
-mazishi yake yalihudhuriwa na waheshimiwa kutoka sehemu tofauti na katika wasia wake kabla ya kufariki alininasihi nisome sana elimu na nipende watu japo kama hawatonipenda.
Wasalaam
Ahmed Ali Sharif Mussa (Mtoto wa mwisho wa marehemu ALI SHARIFF)
Historia nzuri sana na wasia mzuri pia aloachiwa wapende watu japo hawatokupenda....Nimeipenda. RIP - Alli Shariff Mussa.
ReplyDeleteMdau wa Oxford
Asante sana bwana Ahmedi kwa kumkumbuka marehemu na kutoa historia yote hiyo ambayo hata mimi sikuijua. Shariff Othman
ReplyDeleteKUMBE HII TANZANIA AU ZANZIBAR HAKUNA TOFAUTI NA WATU WAKE WANATOKA TANZANIA WANAELEKEA VISIWANI SEMA LABAA NI ILE WARABU NAO KUJA KISIWANI NA KUCHUKUA WAFRICA WENGINE KAMA UTUMWA NA WENGINE KUZAA NAO NAO NA WAINGELEZA NAO KUCHUKUA ZANZIBAR NA WAJERUMANI NAO KUCHUKUA TANZANIA NDIO WAKAWATOFAUTISHA KIDOGO, INAELEKEA MIAKA HIYO KABLA YA HAO WATU WENGINE. WENYEWE WAFRIKA WANAJISAFILIA NA TU MASHUWA TWAO MPAKA VISIWANI.ANETAKA KUWEKA MAKAZI ANAWEKA, ANAETAKA KURUDI ANARUDI NA NDIO MAANA MAJINA MENGI YA ZANZIBAR NDIO MAJINA YA KOO ZA TANZANIA BARA. WAOOO. NI KISEHEMU KIDOGO TUU KILICHOTINGA BAHARINI NA JAMII NYINGINE YA WATU NAO WAKAKIFUTIA ANY WAY, BINADAMU ANAZUNGUKA. lAKINI YAONYESHA WENYEJI NI WAFRICA HARISI,
ReplyDeleteMwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi. Ameen!
ReplyDeleteMwenye enzi Mungu amrehemu. Ameen. Akina Takadiri na Sykes hawakuwa peke yao. Tatizo letu huku bara hatujui historia halisi yao au ya watu wa Zanzibar kwa sababu haielezwi vizuri na hawaitafuti. Ndio maana hata Mchugaji mtikila anatuita wadanganyika. Huwa hakosei ndio ukweli ingawa unauma, hasa vijana wa leo wengi wanaparamia mambo hawajui hata historia ya kijiji anakotoka mtu. Hii ni aibu. Mbowe au Slaa mmoja wao si alisema kwamba Idriss Abdulwakil ni Kihiyo. Hii si aibu. Tusome sio tunakurupuka tu. Humu watoto wanasoma, tusaidiane tuwaelemishe sio tunatoa matusi tu. Elimu sio kwenda shule, Humu humu tunapata elimu. He wadanganyika nye.
ReplyDeleteWatanzania hasa wasomi na wale wasio wasomi sana, kwanini tunasubiri watu wa nje ndio watufanyie vitu, kama kuweka kumbukumbu, utafiti,makumbusho, kujitolea kufanya kitu cha kijamii nk.... sie tunafanya nini...?
ReplyDeleteHasa upande wa shughuli za kijamii zinazohitajika sana sisi wenyewe hatujishughulishi hadi atoke mzungu ndio aanzishe...?
Naona kila kukicha tunafukuzia fedha tuu, jamani kuna vitu na mambo mengine yanafaida kuliko utajiri! Hivi ni bora kumuachia mwanao elimu ilo bora au kumuachia ma pesa?
Daah nimeipenda historia ya huyu mzee. Alikuwa mzalendo na mpigania haki kwelikweli bila hila ndani yake. Hawa wazee ndio wametuwezesha sisi watanzania kufika hapa tulipofika leo. RIP
ReplyDelete