
Mkurugenzi Mkuu wa Radio Karagwe FM Bw. Emmanuel Muga (kulia) akiwa studio na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Col. Fabian Massaw, ambaye hualikwa studio mara kwa mara kujibu maswali moja kwa moja kutoka kwa wasikilizaji wa redio hiyo. Radio za Jamii zimezidi kuenea nchini kote na Radio Karagwe FM ni moja ya redio zinazoongoza mkoani Kagera.
Vizuri sana Karagwe, huu ni mfano mzuri wa kuigwa kwani local news siku zote huwa ni muhimu....
ReplyDeleteSisi tunaotokea Mwanjelwa bado tunasikiliza radio za Dar.. ninajua siku zijazo tutaweza kuwa na uwezo wa kuweka kitu kama hichi..
Brother Michu ahsante sana kwa kuweka habari kama hizi..
Naona huko nyuma kuna chupa ya Serengeti Beer? Vipi watangazaji hupata kilaji kwanza kisha wakaingia hewani?
ReplyDeleteMkuu wa wilya KARAGWE = MASSAWE???
ReplyDeleteHee! Mwanjelwa hakuna Radio?mbona huku Kyela tuna Radio yetu muda mrefu tu sasa tumeshaachana na ushamba wa kusikiliza mambo ya Dar...kwanza wala hatukujui.
ReplyDeleteAnon namba mbili yaelekea umepoteza uwezo wa kuona .ina bidi ukapige One Cup kwa Babu, hiyo chupa inaonekana kabisa ni ya maji, we unasema Serengeti. yaelekea mdau sana wa kilaji hata maji waita pombe.
ReplyDelete