Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Engutoto katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha, wakati alipotembelea Shule hiyo leo kwa ajili ya kufunguwa Jengo la Bwalo wa Wanafunzi, Makamu Rais yupo Mkoani Arusha kukaguwa na kizinduwa miradi ya maendeleo. katikati Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Isidore Shirima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Maabara katika Shule ya Sekondari Nanja Wilayani Monduli, alipokuwa katika mfululizo wa ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Wilayani Monduli Mkoani Arusha leo. kulia Mbunge wa Monduli Mhe.Edward Lowassa na Mkuu wa Mkoa Arusha Mhe. Isidore Shirima.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal katikati, akitembelea mashamba ya kilimo cha mpunga katika mabonde ya Mto wa Mbu Wilayani Monduli, wakati alipokuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo. kulia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.Isidore Shirima
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiangalia mashamba ya kilimo cha mpunga katika mabonde ya Mto wa Mbu Wilayani Munduli, alipokuwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo Mkoani Arusha leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwauliza maswali ya masomo ya physics na kemistry wanafunzi wa Shule ya Sekondari Edward Lowassa Wilayani Monduli, alipokuwa akitembelea majengo ya Shule hiyo leo pamoja na kuangalia maendeleo ya wanafunzi hao. Makamu wa Rais yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya siku nne ya kukaguwa na kuzinduwa miradi ya maendeleo.Picha na Amour Nassor VPO.


Na Penzi Nyamungumi - Arusha

Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal ameutaka ushirika wa wafugaji (RAMAT) wilayani Monduli kutilia mkazo ufugaji wa kisasa kwa maendeleo yao.

Dk. Bilal ametoa rai hiyo jana (Jumatatu) wakati alipokuwa akisalimiana na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi jengo la ofisi ya ushirika huo alipotembelea wilaya ya Monduli wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Arusha.

Aidha katika ziara hiyo Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya ujenzi wa machinjio ya kisasa na kuona mifugo ilivyoboreshwa na vikundi vya wafugaji vinavyounda ushirika huo.

Alisema wafugaji hao wana bahati ya kuwa na machinjio ya kisasa karibu na maeneo yao ambapo watauza ng’ombe kwenye ushirika wao na kuchinjwa katika machinjio hayo na hatimaye watauza nyama kwa bei nzuri.

Alisema katika hali hiyo ya kuwa na machinjio ya kisasa hawana budi kufuga kisasa kwa kutunza mifugo yao.

“Tutie mkazo kwenye ufugaji wa kisasa ili tupate maendeleo. Tuna kiwanda cha kisasa, tutauza ng’ombe kwenye ushirika tutachinja hapa na mtapata bei nzuri,” alisema Dk. Bilal.

Aliwapongeza wafugaji hao kwa kuitikia wito wa serikali wa kutaka wananchi kujijengea misingi ya maisha bora kwa kupitia sekta ya mifugo.

Aliwataka wafugaji ambao bado hawajajiunga na ushirika huo wafanye hivyo sasa kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Taarifa ya ushirika wa wafugaji kwa Makamu wa Rais ilieleza kuwa mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi hiyo ulioanza mwaka 2009 umefikia shilingi milioni 44.8 hadi sasa sawa na asilimia 80 ya gharama zote zinazokisiwa za shilingi milioni 56.1 hadi litakapokamilika.

“Gharama za ujenzi huu inatokana na uchangiaji wa pamoja na ufadhili wa ADF (African Development Foundation) wa shilingi milioni 50.3. Vyama vya wafugaji shilingi milioni 4.5 na Mbunge wetu na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowassa mabati 100,” ilisema sehemu ya taarifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. naona taratibu mzee anajivuta karibu na eneo la tukio, loliondo

    ReplyDelete
  2. Hawa walinzi wa huyu mzee wanavaa kama chadema. Si mhamie tu huko? Au ni ili mkimpeleka mzee Loli kwa babu watu wadhanie ni mzee Ndesa kawapeleka wapiga kura wake?

    ReplyDelete
  3. Hivi hapo yupo nje au ndani? Tushukuru Mugu weather tuliyonayo ndio maana tunaweza kuishi easy easy hivi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...