Picha kulia ni ni Muwakilishi wa East Africa Speakers Beureu ,Paul Mashauri,Mwanzilishi wa mfuko wa ARANYANDE Bwa.Matukio Chuma,Mratibu wa mfuko wa ARANYANDE,Dada Irene Sanga pamoja na Dada Liliani kutoka East Africa Speakers Beureu.

=======  ======  ========

MFUKO WA ARANYANDE WAZINDULIWA JIJINI DAR LEO.

Mfuko wa Aranyande ni mfuko dhana ambao nia na dhumuni lake kubwa ni kukumbushana juu ya jukumu la kila mmoja wetu, kujisikia fahari, kujivunia na kuhakikisha wajibu wake kama Mtanzania haumezwi au kubezwa na shughuli za maisha za kila siku na kusahau wajibu muhimu sana kama Taifa kama ndugu, jamaa, mzazi, rafiki na mwananchi.  Lengo kuu la Mfuko wa Aranyande limejikita kwa makusudi kabisa katika kusaidia nyanja ya elimu ikiwa kama kiungo na chachu muhimu ya kuchochea maendeleo ya kila mmoja wetu lakini pia kama nchi na taifa liitwalo Tanzania.

Neno Aranyande asili yake ni jina la marehemu mama yangu na kuchukua jina hilo kuupa mfuko huu ni kutambua, kusadifu na kuendeleza kazi kubwa sana ifanywayo na kiumbe aitwaye mwanamke ambae kwa hakika kwa muda mrefu amepitia madhila na changamoto nyingi sana lakini nafikiri sote ni jambo lisilo na kificho kuwa kiumbe huyu ni muhimu sana kama nguzo katika familia nyingi mno, kiumbe aliyejaa wingi wa uvumilivu, upendo, ustahimilivu na ambae daima atabaki kuwa alama kubwa ya mafanikio na umoja katika ngazi kuu kabisa ya uwepo wa jamii yeyote duniani yaani familia.  Ni takribani miaka kumi na sita tangu mama yangu aiage dunia hii lakini bado najisikia kama angali uwepo wake ni jana tu, hii ni kwa sababu ya upendo wa dhati, malezi yasiyo ukomo bali wingi wa uhakiki wa maisha ya mafanikio kwa kila aitwae mwanae, ndugu, jamaa ama rafiki na hasa kwa msisitizo katika elimu ili kuhakikisha ukombozi na ueledi kwa kila mmoja wetu.  Aranyande imaanishayo lulu, yenye thamani isiyo ukomo bali wingi wa amani, upendo na heshima. 

Mfuko wa Aranyande ambao nauzindua leo hii si dhana iliyoanza jana au leo bali kwa miaka kadhaa kupitia vituo mbalimbali na kusomesha watoto kadhaa katika ngazi tofauti tofauti lakini imefika kipindi ambacho nimeona ni wakati muafaka kwa kila mtanzania kuamua na kutambua umuhimu wa kujitolea katika kusaidia wale wasio na uwezo ili kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa letu. Si wakati wa kulalama, kulaumu ama kukata tamaa peke yake bali kujitoa, kujitambua na kubwa zaidi kuchukua hatua.  Kama kuna mwenye majukumu lakini yeye akachagua kudharau, kubeza, kuwa na kiburi na wingi wa zenye kukera kauli, haina maana na wala haitosaidia kama taifa kwetu sote kuamua kukaa kimya ama kulalama na kulaumu peke yake bali wengi walio weledi husema muungwana ni kitendo.

Popote tulipo katika dunia hii jadidu tutambue kuwa sisi ni watanzania, kujikana, kujisahaulisha au kuamua tu kusahau kwa kusudi zenye tambo na kebehi haisaidii wala kuokoa taifa leu bali ni sawa na kuwa abiria kwenye chombo na kukaa kimya angali hatari au uongezeko wa matatizo katika jamii yetu hasa kwa wale wasiojiweza ikiongezeka.

Mfuko wa Aranyade ni mfuko utakaotoa angalau ufadhili kwa watoto wawili kila mwaka kwa mwaka mzima katika suala zima la malipo ya masomo ili changamoto tuzipatazo kwa kukosa wazazi, walezi, uwezo, makundi tengwa katika jamii nakadhalika zisiwe chachu ya kutukosesha kile kilicho cha msingi kabisa katika maisha yetu yanatukabili yaani elimu.

Mfuko huu utaratibiwa kwa ushirikiano mkubwa na The East Africa Speakers Bureau amabo hawa ni mabingwa katika nyanja ya uratibu, semina elekezi na zenye wingi wa mafunzo ya nyanja mbalimbali vilevile makongamano na shughuli zifanywazo kwa umakini wa hali ya juu.  Shukrani za kipekee ziende kwao na timu yao yote kwa kukubali kusimamia na kuratibu zoezi hili hasa katika kipindi hiki japo wana majukumu makubwa na mengi lakini mchango wao katika yale yahusuyo ueledi na uendelevu na mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla halina kificho bali wingi wa utekelezaji.

Mfuko wa Aranyande pia na shughuli nzima ya leo haungeweza kuwa mafanikio kama si ushirikiano wa kutosha kutoka kwa msanii nguli, mwenye wingi wa sanaa liyojaa mafundisho, burudani inakishwayo na midundo ya kiasili ya nchi yetu tukufu ya Tanzania, sio mwingine napenda kumwita Shangazi aliyejaa wingi wa hekima na mashairi yale vilivyojipanga vina, Irene Sanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Nakupa big up matukia kwa ubunifu na jitihada zako za kusaidia wasiojiweza

    ReplyDelete
  2. It's very good place for holidays.

    ReplyDelete
  3. Good job Matukio

    ReplyDelete
  4. Way to go Matu..am proud of u

    ReplyDelete
  5. Way to go bro..am proud of you!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...