Mkurugenzi wa African Stars Entertainment Da' Asha Baraka Akitoa maelezo Kuhusu timu ya Saidia Gongo la Mboto UK
Meya wa Halmashauri ya Ilala, Mstahiki Jerry Slaa (kushoto), akisikiliza hotuba ya Meya wa Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Mstahiki Yussuf Mwenda (katikati), kulia ni Asha Baraka
Timu ya Saidia Gongo La Mboto UK wakiwa
katika hatua za mwisho kupakia mizigo

Mdau akiwa kazini
Kazi ya upakiaji ikiendela kwa ajili ya kusaidia
waathirika wa mabomu Gongo la Mboto
Wadau wakijitayarisha kupakia mizigo

WATANZANIA waishio Uingereza Ijumaa iliyopita walishirikiana na bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta Sugu Kisima cha Burudani’ kufanikisha harambe ya kuwachangia waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea hivi karibuni Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.

Akielezea Mchakato Mzima Mkurugenzi wa Twanga Pepeta Asha Baraka mbele ya wageni rasmi Meya wa Halmashauri ya Ilala, Jerry Slaa na Meya wa Halmashauri ya Kinondoni, Yusuf Mwenda alifananua kuwa Timu ya SAIDIA GONGO LA MBOTO UK imetoa misaada katika makundi matatu:
1. Pesa taslim sh milllion moja na nusu
2. Chakula ambacho kitakabidhiwa mapema wiki hii
3. Nguo, viatu, vitabu na vifaa mbalimbali ambavyo vimepakiwa kwenye kontena tayari kwa safari ya kuja Tanzania


Twanga Pepeta ilifanya onyesho maalum Machi 4 mwaka huu katika ukumbi wa Zhong Hua Garden uliopo Mikocheni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam na kupata kiasi cha milion moja zitakazowakilishwa kwa waathirika hao.

Aidha Asha Baraka alisema shughuli hiyo ya uandaaji na ukusanyaji wa michango hiyo kutoka Uingereza iliandaliwa na Shilla Frisch, Jestina George kutoka MISSJESTINAGEORGE.BLOGSPOT.COM, Frank Eyembe na Baraka Baraka wa URBAN PULSE CREATIVE na Bernard Chisumo kutoka Locus Impex Shipping Co.

Pia Asha Baraka Alitoa shukrani za dhati wa wale wote walioguswa na kuweza kutoa michango yao kwa ajili ya kusaidia wahangwa wa Gongo la Mboto na kuwasihi watanzania wote pale walipo kuendela kutoa michango.


Be Cheerful! GOD loves you more than you'll ever know!



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. MFANO MZURI MMETOA WABONGO WA UK,

    ReplyDelete
  2. Mangi wa KiboshoMarch 08, 2011

    Wabeba Mabox hongereni sana sana na imependeza sana

    ReplyDelete
  3. Acheni sasa kuwadharau wa beba box.wantanzania tubadilike, maneno mengi.Hongereni sana Uk mmeonyesha mfano mungu awabariki.

    ReplyDelete
  4. hahahhaahahahhaha e bwana naskia wametoa hayo maboksi ma3 tu halaf wamepakia magar yao ili wapate free ushuru wabongo bwana kufa kufaaana hahhahahahahahhaha

    ReplyDelete
  5. hahahhahahhaha haya kiriwe kaza msul kisombe mbona hubeb wauza sura tu hahahahahhhahahaha, by ngoi bongo

    ReplyDelete
  6. We Anonymous hapo juu unahakika na unacho kiandika hapa au umeamua tu kuzusha kama kawaida yako? Hivi watu mtakuwa lini? Chuki binafsi inakusumbua na lazima kuna lijitu litokee lenye kashfa wakati wote. Hata kama ushuru haulipwi we inakuuma nini? Given the chance ungekataa kutuma vitu vyako. Hebu kuwa kidogo. Kwa kweli napenda sana kuwapongeza hawa vijana kwa kazi waliyo ifanya na wote waliochangia, Mungu awabariki na kuwazidishia. Huu ni mfano wa kuiigwa! Acheni majungu wabongo wa UK mnatia aibu sana.

    ReplyDelete
  7. Ni vizuri kwa Watanzania waishio nje kusaidia nyumbani wakati wa maafa kama haya. Lakini kwa upande wa UK umoja wa kushirikiana Watanzania sio nzuri.Kuna kikundi kidogo tu cha Watanzania wanaoishi London ndio wanaojiita Watanzania halisi. Tupo Wabongo wengi tunaishi hapa UK hatupati taarifa zozote kuhusu vikundi kama hivyo na tunao uwezo wa kuchangia hiyo misaada. Naona bado wengi wana ushamba kuwa usipoishi kwenye mji mkubwa kama London, Coventry, Reading au Luton mlikojazana na kuanzisha Manzese ndogo wengine walio nje ni njaa tu.
    Nasi tuna ndugu huko na tunataka kusaida. Let us have the contacts za kutuma hivyo vitu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...