Habari iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde,inaripoti kwama aliekuwa mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania,Mzee John Luwanda ambaye pia ni Baba wa mpiganaji mwenzetu,Beda Msimbe (pichani) amefariki dunia katika hopitali ya Muhimbili leo mchana baada ya kuugua kwa siku kadhaa.

Kwa mujibu wa Beda Msimbe ambaye ni mmoja kati ya watoto 6 wa Mzee Luwanda,aliewahi kuwa mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania ambaye alistaafu kazi hiyo mwanzoni mwa miaka ya 1990 alikuwa amelazwa katika hospitali ya Muhimbili akisumbuliwa na kisukari huku akifanyiwa uchunguzi wa kansa ya kibofu cha mkojo.

Mtoto wake huyo alisema kwamba madaktari walimwambia kwamba baba yake alikufa kutokana na ugonjwa wa uti wa mgongo.

Mzee Luwanda ambaye atakumbukwa zaidi na watu wa vikundi vya sanaa kwa uandalizi wa michezo ya kuigiza ya radio.

Mara baada ya kustaafu Marehemu Mzee Luwanda alikuwa anaishi katika kijiji cha Goba akilima bustani na kufuga mifugo.

Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake Goba kijijini na anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi wiki hii.

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi.

- Ameen

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. pole beda msimbe.

    ReplyDelete
  2. Pole sana Beda.Tunamuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mzee mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  3. RIP sekulu Luanda

    ReplyDelete
  4. Pole sana mpiganaji. Tupo pamoja katika wakati huu mgumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...