Salaam Mr. Michuzi,
Napenda kukupongeza kwa kazi unayoifanya ya kuelimisha jamii kupitia huu mtandao. Nipo Marekani lkn haipiti siku bila kuupitia. Msaada ninaoomba ni kwamba kuna kiwanja eneo la Bunju kina hati miliki na ukubwa wa sq meters 1638. Nimeambiwa bei yake ni million 17, tafadhali naoma wadau wanifahamishe kupitia blog yetu ya jamii kama ni sahihi au naibiwa.

Kazi njema,

Natanguliza shukrani,

Mama Jr.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. He! nackia kuna jamaa wanatoka nchi moja ambayo haijawa na amani wala Serikali imara kwa zaidi ya miaka 20 sasa wananunua viwanja Dar kama njugu wanamwaga dola kinoma na tulivyojiachia bila kujali usalama wetu na huko tuendako jamani naogopa sana! Na wewe hicho kiwanja chako wakickia tu - ujue huna chako watabeba hata kwa Milioni 50!!!

    ReplyDelete
  2. ajaibaga jogoo la malkia flani uyu kweli kabla hajawa mbunge. katoa wapi wimbo mziri ivi. ujumbe wa kweli.

    ReplyDelete
  3. Bwana Amerika nakushauri ufanye mambo yafuatayo:
    Nunua tiketi ya ndege njoo Dar ukione kiwanja na kumaliza mambo yoote ya kisheria. Nakushauri usinunue ardhi kupitia mtandao.

    ReplyDelete
  4. Viwanja vingi maeneo ya Bunju Millioni 3-5 mwisho navyojuwa mie ila pengine jamaa Kimepimwa kimeinavyotakiwa kilakitu Ngejela

    ReplyDelete
  5. Mama Jr, hiyo ni 0.4 ya Acre, na nadhani kulipia hiyo pesa ni wehu. Ukiongeza 4 Million unapata 4050 Sq meters maeneo ya Mivumoni au Madale.

    Japo development bado sio kubwa lakini potential ya kugrow ipo kubwa sana.

    Kwa wale mnasema apande ndege huku hatufanyi kazi tigo kusema nakwenda home. Lazima uchukue muda kumuaga muajiri.

    Maana ni kwamba acre moja maeneo hayo ni Million 42? That is insane

    Mdau wa USA

    ReplyDelete
  6. we mama vipi bwana marekani kama una milion 17 that means una uwezo wa kukata tiket na kuja kukifatilia hicho kiwanja na kujua uhalisia wake kuliko kuuliza watu kwenye michuzi viwanja kinaweza kuuzwa bei yeyote inategemea na muuzaji soko huria mama unaweza kuuziwa hata milion 100 hebu acha mashauzi nenda bongo kafanye legal proces usije rudi kwa michuzi uanze kutulilia umeibiwa hela za box kuosha wazee tunajua sio kazi ndogo

    ReplyDelete
  7. Mi nakushauri uje mwenyewe dar na umtafute mwanasheria ambaye atakusaidia kufanya huo ununuzi hasa ktk suala la kumjua mmiliki halali wa hicho kiwanja.Weingi wanaingizwa mjini.Ukiwa na mwanasheria anajua hatua za kufanya kuhakikisha hauingizwi mjini.

    ReplyDelete
  8. Mama NancyMarch 17, 2011

    Mama Jr. Hiyo bei ni halali kabisa tene wamekupunguzia sana. Mie nilinunua mwaka 2009 sq meter 1296 Bunju kwa milioni 18.Last month kuna m2kanunua kiwanja kwa mil 40 karibu nami. Hivyo vya mil3 sjui 5 ni kweli vipo tena vingi tu ila sasa ujue kabisa kuwa havijapimwa. Ushauri wangu: kama unauhakika na huyo m2 mwenye title deed ni bora zaidi x 100 na bei iko poa kabisa.(Avoid udalali)

    ReplyDelete
  9. nyieee kwani kupima kiwanja bei gani hadi mseme ati km kimepimwa m17 ni halali, the same size hakijapinmwa m3-4?? ukweli ni kuwa tz ardhi inauzwa hovyo, unaweza mpata wa one acre imepimwa kutokana na dhiki zake ukauziwa m5 pia!

    ReplyDelete
  10. Mzee wa BunjuMarch 17, 2011

    Mama Njoo haraka kabla hakijaenda bunju viwanja barabarni mpaka milioni 60 jirani yangu kanunua viwili kwa 80 juzi tu pale kwa jumbe Bunju A, mimi mwenyewe naish pale toka mwaka 2004 na kwa kweli nilibahatika kwa bei kiduuuchu kakini kipindi kile niliona kama nimegongwa sana, fanya fasta kabla mzaramo haya shikwa masikio

    Mzee wa Bunju

    ReplyDelete
  11. MAMA Jr,

    Kiwanja cha Binji kwa bei hiyo ni halali kabisa, ispokuwa nakushauri ufuatilie ardhi ili kukihakiki uEsije kuuziwa mbuzi kwenye kiloba,

    ACHANA NA NARUDIA TENA ACHANA kununua viwanja ambavyo havijapimwa maana siku hizi utasikia tu serikali inataka kuanzisha mradi eneo fulani na ukiangalia ni hayo ambayo hayajapimwa! SO BE CAREFUL mwenzangu, usisikilize hawa watu wa viwanja visivopimwa utajuta! mwenzio yalishanikuta!

    Good luck ...ila hakiki ardhi kwanza na hizo sq mtr ni kiwanja kikubwa sana hicho "Low density"..go for it ..but kwanza hakiki ardhi mama matapeli wengi

    ReplyDelete
  12. Mdau unayesema hiyo ni robo eka ukweli hujui ukubwa wa viwanja na wacha kumdanganya mwenzio. Robo eka ni viwanja vyenye ukubwa wa 400sq mpaka 550 sqm, navyo viko kwenye high density. Na viwanja kuanzia 600sqm mpaka kwenye nafikiri 900 hivi viko medium density na kuanzia 1000sqm ni Low density, hicho kiwanja kitakuwa Super low density na sidhani kama vile vilivyopimwa kwenye mpango wa serikali kwenye mradi kuna chenye ukubwa sina uhakika, ila muulize hicho kiwanja kilipimwa wakati wa mradi wa viwanja elfu 20 au alijipimia mwenyewe? Ila pia inawezekana vipo vikubwa namna hiyo ambavyo vilikutwa na vibanda ndani yake vikabakishwa hivyo hivyo. Ila kwa bei hiyo anayosema kama ni kweli ukubwa huo basi ni bei halali.

    Kwanini usitumie kampuni ya survey ikakuchekia kama kweli hicho kiwanja kipo? Wao watakachofanya ni kwenda kucheki ardhi kama hicho kiwanja kipo na hiyo hati ni ya huyo mwenye kiwanja kwa kufanya search. Tafuta Geomatics Engineering Consultants Ltd kwenye mtandao, kisha wasiliana nao. Ofisi zao ziko mnazi mmoja.

    ReplyDelete
  13. Mama Junior hebu nitumie contacts za huyo muuzaji nifuatilie vizuri then ntakufahamisha matapeli wengi siku hizi.

    ReplyDelete
  14. Ivi kwa nini watu wengine mnakuwa na kejeli na maneno yasiofaa kwa watu wanaoomba msaada humu bloguni? kama mna stress si mtafute njia nyingine ya kuzitoa kuliko kutoa kauli za hovyo humu? naomba tuwe wastaarabu jama

    ReplyDelete
  15. Mama Jr usikubali kuwatafuta hao Geomatics Engineering Consultants Ltd wewe nenda ama tuma mtu wako ardhi akacheki halafu aku-inform wewe. Ukiwatuma waweza poteza bahati yako yaani wakakuzunguka. Mimi yalishanikuta, hata mawakili wengine hivyo hivyo wamwomba ushauri yeye anaongeza hapo 0.5M anachukua yeye ama anamtafuta mteja kwa bei ya juu kidogo.

    Vile vile ardhi ukalipie kabisa official search kama Tshs 5,000/= hivi wakupe risiti. Waweza wawezesha ili wafanye haraka kidogo, yaani badala ya kusubiri wiki mbili wafanye within days, baada ya hapo chukua hatua kufuatana na taarifa hizo hasa ukiwa na official search na umeishakubaliana naye ndipo WAKILI aingie, usikubali option wanayotoa matapeli wengi eti twende mahakamani hasa zile za mwanzo.

    Kwa BEI ni sawa kwa maeneo hayo kama ana title deed, kama akijapimwa ogopa kama ukoma
    Huo ni ushauri tu.

    Observer

    ReplyDelete
  16. mimi ni mkazi wa Bunju. aliyekwambia hivyo anakuibia viwanja vyenye hata maeneo hayo vinaanzia milioni 20 na kuendelea lakini haipungui kuwa na makini. mdau

    ReplyDelete
  17. mama jr pia hata search siku hizi ni muhimnu lakini nina ushahidi kwamba watu wanauziwa kiwanja kinachomilikiwa na mtu mwingine na ukienda kusearch wilayani hasa kinondoni au wizarani unakuta safi lakini baadaye mnakutana mahakamani unaambiwa umenunua kiwanja cha mtu bila mwenyewe kuwa na taarifa, ndiyo bongo yetu hii ilivyo sasa!-mdau martson

    ReplyDelete
  18. Ni halali mama, chukua!
    Mama Jr, epuka kumtumia middle person/kampuni yeyote kwenye hiki kiwanja, kama umeshakubaliana na mwenye kiwanja ni powa kabisa. Tena hata usije ukatoa contacts zake, kwani hao middlemen ndo huwa wanawazunguka watu baadaye.
    katika kununua jua yafuatayo.
    1.Omba number ya kiwanja na block, nenda ardhi for 'Title search'(inachukua mpaka siku 14, ila ukiwapa hela kidogo, hata siku tatu wanamaliza.
    2.Then kama ni halali, mkubalianae na muuzaji 'nani atalipia kodi? i mean capital gain TRA, kihalali muuzaji ndo anatakiwa kulipa, kama mtakubaliana ulipe wewe basi akupe discount.(muhimu sana hii)msipokubaliana ukishamlipa utakuwa ni mzigo wako, na sio mzigo mdogo mama.Maana TRA wataki-value katika market price ya sasa, ambayo yaweza kuwa 35ml, then utalipia 10% ambayo ni 3.5m
    3.Tafuta mwanasheria muuziane, then uanze process za kubadili jina mara moja, (utaanzia Kinondoni municipality, then TRA, then Ardhi) kama six months waweza kumaliza kazi yote!

    ReplyDelete
  19. Mama J,

    Hio bei ni sawa, IWAPO ni cha mradi wa viwanja 20,000. Kama sio, uwezekano wa kutapeliwa ni mkubwa! Maendeleo eneo hilo yanaenda kwa kasi na bei zitapanda kutokana na upanuzi wa barabara ya mwenge-wazo hill ambao umeanza.
    Aidha, binafsi nauza kiwanja changu Mbweni JKT ambapo ni eneo la karibu zaidi ya huko Bunju,.Kiwanja cha Mradi na clean title, bei tutaelewana, sasa niko ulaya ila nitaenda bongo mwezi ujao, unaweza kuni sms mobile +33627559439 au home +33469550853 (after 19hrs)
    Mdau

    ReplyDelete
  20. Nionavyo mimi bei ni ndogo. Wahi mapema kabla hakijawahiwa.

    USHAURI
    1. Pata jina kamili la muuzaji na uliandike mahali.
    2. Mtume mtu unayemuamini akafanye utafiti ardhi wajina kamili la mmili wa hicho kiwanja.
    3. Jina la mmiliki likiwa sawa na ulilopewa anza taratibu za kutafuta wakili kwaajili ya manunuzi.Vinginevyo usijeuziwa kiwanja na tapeli au chenye mgogoro wa kifamilia UTAJUUTA!!!

    Ila siku hizi Ardhi Wanahitaji picha ya muuzaji namnunuzi wa kiwanja na sahihi zao. Unaweza muamini ndugu na akaja kukukana na kiwanja kikawa mali yake.

    ReplyDelete
  21. Ni heri uende Bongo uangalie mwenyewe...Hiyo hela ni nyingi sana. Mimi nilikata tamaa ya kununua kiwanja Dar kwa vile kila siku nilikua naona hizi bei watu wanazosema huku nikajua sitaweza kabisa. Nilinunua kiwanja uchaggani lakini baadaye nikaamua kwenda mwenyewe kuangalia. Do listen but don't take all the advices here to make your final decisions....Hivi unajua maana ya social comparison? I guarantee you 99% ya watu wanaokwambia hiyo bei ni poa kabisa hawajanunua hata kiwanja au kama wanacho hawajalipa hiyo hela...Mimi nimenunua kiwanja Dar sehemu nzuri kimepimwa , kina title na imetumia lawyer na nililipa million 4 na some change tu,. Narudia tena million 4 tu. Kama ni ndugu anakuambia hiyo bei mwache mbali , kama ni rafiki don't walk run. Watu wakijua uko sehemu ya nje ya nchi wana price up so much.

    Wewe nenda tafuta viwanja kama vinne halafu anagalia nyumba zilizojengwa jirani ni za gharama gani. Wakikupa price yao wewe wape unayojua ni halali. Akikataa ondoka..Nilifanya hivyo kwa viwili cha tatu nimeondoka kesho yake wananipigia simu na kuniambia wamekubali ile hela niliyo waambia...Usisikilize mambo ya huku kwa mablog ya watu kuandika under the umbrella of anonymous. 99% of what we see or read is not true...Nenda kaangalie mwenyewe. Viwanja watu wanajiuzia tu bila kujua thamani yake basi na wewe kama unaenda kichwa kichwa watakubamiza hawa kweli...

    Good luck

    ReplyDelete
  22. Anonymous 7:28, ni kweli unapongumzia due diligence kwenye kununu viwanja, lakini dar es salaam kuna viwanja kuanzia laki 5 mpaka 1 bilion (tena unalipa kwa forex sio madafu), so unaposema umenunua kiwanja milioni nne ni bora ungemsaidia mama J kwa kumwambia ni wapi umenunua iko kiwanja,maana kwa dsm hio bei ni ya shamba sio kiwanja, kwa upande wa njia ya bagamoyo ni past bunju kuelekea bagamoyo, kigamboni hakuna bei hio mpaka upite gezaulole, kimara kwenyewe ndio sijui wapi, labda ukaribie kibaha,

    what determies the price ni level of development, surrounding n.k n.k, most of the upcoming middle class areas, kibada,mbweni, bunju, kimara kote prices ziko juu, au iko kiwanja cha uchaggani ndio milioni 4? labda huko sio dsm middle class area ambayo uta expect mama Junior akitoka huko aliko sijui ulaya ndio akakae huko,

    unafikiri ataenda kukaa kwenye squatters ambako ata hakuna parking?au ataenda kukaa uswahilini next house bar inapiga kelele mpaka asubuhi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...