Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu(Kulia) akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo ya Viwanda UNIDO Bw Emanuel Kalenzi (Kushoto). Kushoto kwa Bw Kalenzi ni Bi Grace Bilingeki wa UNIDO. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri mapema leo.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Lazaro Nyalandu, leo amefanya mazungumzo mafupi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda UNIDO hapa nchini Bw Emanuel Kalenzi.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi ya Naibu Waziri Nyalandu, na kuhudhuriwa na mkurugenzi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi Eline Sikazwe na Mkurugenzi Msaidizi Mhandisi Elly Palangyo.
Pamoja na mambo mengine, mazungumzo hayo yamejikita katika mipango na mikakati mbali mbali ya Wizara na Shirika hilo yenye nia ya kuongeza ufanisi wa sekta ya viwanda hapa nchini.

From my heart, nafurahishwa sana na juhudi za mh Nyalandu, namuombea heri ili arejeshe matumaini ya watanzania. Wasiwasi wangu ni wivu na fitna katika siasas za Bongo, hakawii kuzuliwa jambo, kama walivyomfanyia Magufuli.tanzania ina mambo. Nyalandu songa mbele
ReplyDeleteHiyo office with that view huwezi kujua uko bongo...mweeee bongo tambarare....
ReplyDeleteLazaro na wewe hebu weka Big Flat Screen hapo kama ofice ya Ngeleja. Sasa hako ka TV si utakuwa huoni kabisa? Ila kazi nzuri chapa kazi acha siasa.
ReplyDeleteClassmate KSS.
Ofisi ndogo sana hii, kwa mtu kama Nyalandu aliyesoma Marekani anaelewa mambo ya space. It is very small and very uncomfortable. Good luck making a deal with Americans in that small (studio) office.
ReplyDelete