Mshiriki wa mchezo wa kuendesha baiskeli kutoka nchini Hispania Joan Menendez Granados (wa pili kushoto) akimkabidhi jezi na mipira 15 naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ikiwa ni mchango wake kuisaidia timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars) leo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia ni Bw. Muharrami Mchume mjumbe wa kamati ya Olimpiki (kwanza kushoto), baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars na Bi. Juliana Yassoda Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo.
Naibu waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akipokea mipira kutoka kwa Mshiriki wa mchezo wa kuendesha baiskeli kutoka nchini Hispania Joan Menendez Granados (wa pili kushoto) kwa lengo la kuisaidia Timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu ( Twiga Stars) na pia kutambua uwezo wao katika ushiriki wa michezo mbalimbali ya kimataifa leo jijini Dar es salaam.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...