Baada ya taarifa za tiba inayotokana na 'kuoteshwa na Mungu' inayotolewa na Mchungaji Mstaafu Masapile wa Samunge, Loliondo, Arusha kuenea, tukashuhudia kijana mwingine toka Rombo, Kilimanjaro akisema naye ametokewa na 'Bikira Maria' ili kutibu kwa kutumia mti fulani na muda si mrefu akatokea kijana wa Mbeya akisema naye alitokewa na mama yake ndotoni, wote hao wakipewa matibabu ya magonjwa sugu, hatimaye safari hii ameibuka mwingine mkoani Tabora akisema naye anatoa dawa inayoponesha.


Mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Uzunguni kata ya Malolo mjini Tabora, ametangaza kupata uwezo wa ajabu wa kutibu magonjwa sugu kwa kutumia mti shamba na maombi maalum ya kidini.

Tayari mamia ya watu wamejitokeza kupata tiba kutoka kwa mwanamke huyo, ambaye awali alikuwa mfanyabiashara ndogo ndogo, alianza kutoa tiba hiyo kiasi cha wiki mbili zilizopita, ambapo ameweza kumtibu kijana mmoja mwenye matatizo ya akili na ububu.

Mwanamke huyo Magreth Nestory (40), ambaye ni mkazi wa mjini Tabora, amekuwa akitoa kikombe kimoja chenye ujazo wa mililita 300 za maji huku kwa gharama ya shilingi mia tano (500) dawa husika ikiwa haina radha maalum, na hajabainisha inatokana na mti gani.

Hata hivyo kilichosababisha watu wengi zaidi kujitokeza kuitumia dawa hiyo ni kitendo kilichomfanya kijana mmoja aliyekuwa hawezi kusema kupata uwezo wa kusema mara baada ya kuitumia dawa hiyo, ambapo pia ilimfanya apone matatizo ya ugonjwa wa akili.

Mwanamke huyo amesema chanzo cha yeye kutoa tiba hiyo ni kisa kilichompata mwanamke mmoja katika mtaa wa kanyenye mjini hapa, ambapo alipotelewa na mtoto huyo na baada ya kumtibu na kumfanyia maombi mtoto huyo alipatikana akiwa hai kama alivyokuwa ameahidi.

Alisema baada ya kuichimba dawa hiyo walijitokeza watu wa kuinywa kwa ajili ya kutibiwa maradhi mbali mbali ikiwa ni pamoja na maradhi sugu tiba ambayo amekuwa akiitoa kwa gharama ya Shilingi mia tano tu, alisema ndiyo mapenzi ya Mungu.

Hata hivyo aliwataka watu wanaotumia dawa zake kwa ajili ya kupona maradhi yanayowasumbua wanapaswa kuangalia afya zao mara baada ya siku saba baada ya kutumia dawa hiyo. Baadhi ya mashuhuda walisema dawa hiyo inatibu maradhi ya kisukari, ini, moyo, figo, kansa na UKIMWI.

credit : Sunday Kabaye, Tabora

from: http://www.wavuti.com

Kwa taarifa rasmi ya Serikali kuhusu dawa ya Babu wa Loliondo
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Safi sanaaaaaaaaaaaa................!!!!!!!!!!!!!! hizi ni zama za vikombe tuu na vikombe viendelee kudumu. Vikombe viendelee kudumu kwa jina la yesu mpaka "mardhwi" maradhi sugu yote yatoweke.

    tehetehetehehehetehetehetehe

    ReplyDelete
  2. Brother Michuzi,sasa imetosha hawa watu imekuwa kama mchezo,tafadhari naona jina la Mungu linatumiwa vibaya na sisi wanadamu lazima tuheshimu na kumuogopa Mungu,Amen

    ReplyDelete
  3. KAzi ipo !!!!

    ReplyDelete
  4. Kawaida yetu wabongo ku-copy na ku-paste. Akianzisha mtu kitu basi watu wengi huiga. Grocery, Bakery, Pharmacy, Boutiques, vijana wa kiume kuchoma vitumbua kwenye stand za dala dala nk...

    ReplyDelete
  5. Hao wa sasa wote ni feki, Mzee yaani Babu hata siku moja hakujitangaza, mimi naona kuna kampeni inafanywa watu wajitangaze ili kumaliza nguvu za babu lakini nakwambia Babu yuko juu tu.

    Hata wakipandikiza mikoa yote watu wakajitangaza basi waache tu. Lakini Babu yupo juu. Tofauti ya Babu yeye akujitangaza na wapo watu kibao mpaka wazungu wametoa ushuhuda kuwa wamepona

    Babu yuko juu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...