Afisa mwandamizi wa idara uhusiano na huduma kwa wateja Shirika la Taifa Hifadhi ya Jamii NSSF Bw. Juma Kitu akimkabidhi tiketi ya Ndege Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo nchini TASWA Bw. Maulid Kitenge kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo Duniani AIPS unaofanyika Korea Kusini kuanzia March 22 hadi 27 mwaka huu.Kitenge ataiwakilisha TASWA katika Mkutano huo.

SHIRIKA la Hifadhi ya Jamii (NSSF), jana lilikipiga tafu ya sh milioni 3 Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), ili kukifanikishia kushiriki kongamano la waandishi wa habari duniani litakalofanyika Machi 22 hadi 27 Korea Kusini.

Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam kati ya Ofisa Habari Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu, na Makamu Mwenyekiti wa TASWA, Maulid Kitenge, ambaye ndiye atakayekiwakilisha chama hicho katika kongamano hilo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Kintu alisema fedha hizo zitagharamia tiketi kwa ajili hiyo, hasa baada ya kutambua mchango wa waandishi wa habari katika nyanja ya maendeleo.

Kintu alisema Kitenge ni mmoja wa wadau wanaoitangaza NSSF katika nyanja ya maendeleo hapa nchini.

Naye Kitenge kwa upande wake, aliishukuru NSSF kwa msaada huo ambao utamwezesha kwenda na kurejea katika kongamano hilo ambapo anatarajia kuondoka nchini Machi 21 huku akiahidi amedhamiria kuwaunganisha waandishi wa habari wa Tanzania na wengine.

Kitenge alisema Kamati ya Utendaji ya TASWA, pia itampa mapendekezo ambayo atayawasilisha katika mkutano huo.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando ‘Mgosi’, aliishukuru NSSF kwa msaada huo, ingawa waliomba katika kipindi cha muda mfupi.

Mhando alisema, katika kongamano hilo Kitenge ataambatana na Katibu Msaidizi, George John, na kutoa wito kwa wadau kumsaidia naye afanikishe safari yake hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...