Makipa wa Simba wakiwa mazoezini
uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo

Piha na habari na Woinde Shizza,Arusha

Timu ya Simba ambayo ilikuja jijini hapa majuzi kwa ajili ya mechi baina yao na wenyeji wao AFC wa jijini hapa ambapo katika mechi hiyo timu hii iliweza kuibuka kidedea mara baada ya kuwafunga wenyeji magoli 2-0 imeweka kambi ya siku tatu jijini hapa ili kujifua kwa ajili ya mchezo baina yao na mabingwa wa Afrika Tp mazembe huko Kinshasa katika mchuano wa klabu bingwa wa bara la Afrika.

Akiongea na gazeti hii kocha msaidizi wa timu ya Simba Amri Saidi alisema kuwa wameamua kukaa jijini hapa kwa ajili ya kufanya mazezi makali ili waende kufanya vyema huko nchini kongo ambapo wanaenda kukutana na timu ya Tp Mazembe.

Alisema kuwa japo kuwa wameona uwanja ni mbaya lakini pia hali ya hewa imewaridhisha ndio maana wameamua kubaki hapa ili wachezaji waweze kuzoea hali ya hewa kwani hali ya hewa ya nchini Congo haina tofauti na hali ya hewa ya jijini Arusha.

“unajua hapa hali ya hewa ni nzuri sana ndio maana tumeamua kubaki hapa kupiga zoezi hadi hiyo alihamisi ambayo tunaondoka na tutaenda Dar kuchukuwa usafiri na kuondoka kwenda kukabiliana na Tp Mazembe.

"Pia uwanja huu umetupa taabu sana wakati wa mechi kwa kuwa ni mbovu lakini kwa mazoezi ni mzuri kwani iwapo tukifanya mazoezi katika uwanja mbovu tukienda kule tukikuta mzuri basi wachezaji watapata nafuu kwani watakuwa wamezoea na pia tukifanya mazoezi kwenye uwanja mbovu tukakuta uwanja mbovu pia watakuwa hawapati shida kwa kuwa watakuwa wamezoea”alisema Saidi

Alisema pia wamefurahia kambi nzuri ambayo wameshukia hivyo waomena ni vyema wakiendelea kufanya mazoezi hapa na wanaimani kutokana na mazoezi haya wakienda uko watashinda na watarejea kwa ushindi wa kishindo japo kuwa ni ugenini.

Saidi alisema kuwa pia anapenda kutumia nafasi hiyo kuwashukuru washabiki watimu ya Simba wa mkoa wa Arusha pamoja na washabiki wa mpira kwa ujumla kwa jinsi walivyo wapokea na kuwaonyesha fadhila na amehaidi kulipa fadhila hizo kwa kufanya vyema katika mechi ya Tp Mazembe ambayo wanaenda kucheza.

“napenda nichukue nafasi hii kuwashukuru washabiki wa mkoa wa Arusha kwa jinsi walivyotupokea na kutufadhili hatuna cha kuwalipa bali watazilipa kwa kufanya vizuri na kurudi na matokeo mazuri katika mechi hiyo ambayo wanaenda kucheza kongo”alisema Saidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. OFCOURSE WANAJUA NI KICHAPO TU, SEMA WANAJRIBU KUPUNGUZA IDADI YA MAGOLI.

    ReplyDelete
  2. WASISAHAU KWENDA KWA BABU.

    ReplyDelete
  3. mnyama lazima alale si chini ya goli 4 kutoka kwa mzembe,wamezoea kubebwa katika league ya vodacom na kununua mechi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...