
Kampuni ya Global Publishers ikishirikiana na Clouds Media Group inapenda kuufahamisha umma wa watanzania kuwa wameandaa tamasha la wazi na la bure lililopewa jina la “TAMASHA LA UZALENDO: TANZANIA KWANZA, SISI SOTE NI NDUGU”. Tamasha hili Kubra, linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya tarehe 26 Machi, 2011 katika viwanja vya Biafra, Kinondoni Dar es Salaam kuanzia, saa 5:00 asubuhi hadi saa 12:30 jioni.
Madhumuni ya tamasha hili ni kuwakumbusha watanzania umuhimu wa kuishi pamoja kwa upendo na amani bila kujali tofauti zao. Vilevile kuwahamasisha kuipenda nchi yao na kupendana kama binadamu na kuweka uzalendo mbele kwa maslahi ya taifa. Tamasha hili linakadiriwa kujumuisha watu kati ya 20,000 hadi 25,000 wa rika tofauti na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa makampuni na taasisi mbalimbali wanaoheshimika na jamii, ambao siyo wanasiasa. Kupata habari kamili na mapicha kibao ya tamasha hili la aina yake
BOFYA HAPA
wapi ntapata cd za Galinoma?
ReplyDelete