BENKI ya Rasirimali Tanzania (TIB) imetoa vyakula na mahitaji mengine mbalimbali yenye thamani ya Sh. Mil 4/= kwa waathirika wa mlipuko wa mabomu eneo la Gongo la Mboto, Dar es Salaam.

Vitu vilivyotolewa na benk hiyo ni pamoja na unga wa Sembe, Mchele, Unga wa
Ngano, Mafuta ya Kula ,Sukari, Chumvi,Maharagwe, Sabuni na Nguo.

Mkuu wa Mpango Mkakati na Mahusiano ya Benki Jaffer Mlachano alikabidhi vitu hivyo kwa niaba ya benki kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mecki Sadiki ambapo alitoa rai kwa taasisi nyingine kama wao pamoja na wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kusaidia waathirika husika.

Alisema msaada huo ni katika kuthamini utu wa watanzani wenzao waliopatwa na mkasa huo ambao kwa namna moja au nyingine ni nguvu kazi ya taifa hivyo
wanapaswa kufarijiwa kwa kuwapa msaada.

“Tumesikitika na kuguswa kwa namna ya kipekee na tukio lililowapata wenzetu nasi kama miongoni mwa wadau tunatoa msaada wetu wa vyakula na vitu vingine na wale waliojeruhiwa tunawaombea wapone haraka,”alisema

Kwa upande wakeKaimu Mkuu wa Mkoa aliishukuru benki hiyo na kuiomba kuongeza tena msaada mwingine kama uwezo utawaruhusu kwani mahitaji bado ni mengi.

“Tunawashukuru kwa jinsi mlivyoguswa na kuamua kujitolea kwa kiasi
mlichoweza,lakini bado tunatoa rai kwenu na kwa wadau wengine kujitolea zaidi endapo uwezo unawaruhusu kufanya hivyo kwani mahitaji bado ni mengi”, alisema
mkuu huyo.

Alisema pamoja na watanznaia kuonyesha moyo wa kujitolkea kwa kadri uwezo
ulivyowaruhusu lakini bado Serikali inaamini waathirika husika wataendelea
kuishi kwa kutegemea misaada hiyo kwa kipindi kirefu kijacho kabla ya kurudi
katika hali zao za kawaida kimaisha hivyo wadau bado wanaombwa kujitokeza
kusaidia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...