Mwenyekiti wa TWAA (Tanzania Women Of Achievement Awards),Mama Sadaka Gandhi akizungumza usiku huu katika hafla ya Tuzo mbali mbali kwa wanawake wenye taaluma mbali mbali zilizotolewa katika ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar.
Mwanzilishi wa Mtandao unajihusisha na utoaji tuzo kwa Wanawake wenye Taaluma mbali mbali hapa nchini (TWAA),Irene Kiwia akizungumza katika hafla hiyo usiku huu katika ukumbi wa Mlimani City,Jijini Dar ikiwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 100 ya mwanamke duniani.
Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Caroline Ndungu akimtabidhi tuzo ya TAALUMA (Professional)Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Mwamvita Makamba.Meneja Masoko wa Home Shopping Center,Bi. Fatma (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi pamoja na tuzo,Bi. Khadija Mwanamboka alieshinda tuzo ya Social Welfare.

kwa picha zaidi

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Wakati nasoma hii mkuu, mawazo yangu yalikwenda mbali sana, nikamuwaza mama mdogo, shangazi, binamu hata dada au jirani yetu kule kijijinii ambao wanataabika na jembe la mkoni, ambao wanahangaika kutafuta majani ya ng'mbe , ambao wanahangaika kutafuta kuni, kkwasababu kuni kwao ndio `moto' ndio mwanga. HAWA WATAPEWA TUNZO NA NANI?
    Labda ipo siku dunia itabadilika, kijiini kuwe na neema kama mjini, na walio kijijini wataonekana, ...sijui ni lini. Tunaishia kusema `mwenye nacho, ataneemeka zaidi'
    Hili niwazo tu mkuu katika kushadidisha siku hiyo muhimu ya wanawake. Sio kwamba napinga hizi tunzo, hapana tuzo hizo ni muhimu na ndio mwanzo mzuri...kwani wanaonekana , wanajulikana na juhudi zao tunaziona, `ILA WAPO WENYE SIFA KAMA HIZO NA ZAIDI , NASEMA NA ZAIDI KWASABABU MAISHA YAO, ....NI MTIHANI...MLISHAWAHI KUISHII NA UJI WA CHUMVI...? Mtoto ananyeshwa uji wa chumvi, ili asilie angalau atulie mama akabangaize, mtoto mgongoni, kuni kichwani jembe begani...huyu mama atapewa TUNZO NA NANI?
    Mkuu samhani nimejisahau nikadhani nipo kwenye blog yangu. Tutembeleane mkuu!
    KWAHERI MKUU

    ReplyDelete
  2. MDAU HAPO JUU UMEKUWA NA MAWAZO KAMA YANGU, MIE NAPINGANA SASA NISHAONA HIZI KAMA ZA UMOJA WANAWAKE UMEKUWA BINAFSI, HAWA SAWA WANASAIDIA ILA NAO WASIPEWE WAPEWE WAKINA MAMA WANALIMA VIJIJINI MAUSWAZI KUNA WAKINAMAMA WANAJITUMA, KUNA WAKINAMAMA AU KUNA WAKINADADA WALIKUWA WANAFANYIWA VIBAYA NA WAUME ZAO AU BABA ZAO KUBAKWA KUNYANYASIKA WAMEPATA NAFASI WANASAIDIA JAMII MTAANI HAO NDIO WAKUPEWA... WADAU MNAONAJE MZ.

    ReplyDelete
  3. nakubaliana na ww ikiwa huu ni mwanzo tu basi iko siku tutafika kijijini na kumjali mama anaefuata maji kwa umbali mrefu, anechanja kuni anaelima kwa jembe la mkono na mengine mengi ila kwa sasa ni huku mijini ambako wako ambao mchango wao tunauona kama mwamvita, bila chuki kwa mwanamke mwenzangu nampa hongera sana kwani utandani dada huyu anafanya kazi ya kusaidia jamii na sio Vodacom au anafanya kazi kitengo cha maafa! au!! ukweli anajituma na anastahili, ukiachia yy ni msichana, mama, mke na muajiriwa lkn ameweza kubalalce yote na jamii ikaona anachokifanya.ILA NAKWAZIKA SANA NA WATOA HIZI TUZO NAOMBA MSIZIFANYE ZIONEKANE NI ZA WATU WA TABAKA FULANI HASWA PALE UNAPOAMBIWA KIINGILIO $100 kwanza ni aibu tunapo encourage matumizi ya $ wakati currecy yetu ipo kwa staili hii uchumi utapanda kweli?? pili mimi kama mimi ni lini nitapata nafasi ya kushiriki kiapato changu cha chini?? mnawaona vp wajasiriamali wadogo wadogo amabao tumeona mwanzo wao na sasa wako mbali. anyway naona sitomaliza. TUNAOMBA ZIWE TUZO ZA KWELI NA SI BIASHARA YA KUNUFAISHA WACHACHE

    ReplyDelete
  4. Hello,
    Namsapot sana emu-three, kwani wanawake ni wa kijiji huwezi kuniambia mwanmke amekaa anakula kilaini ameacha sehemu kubwa ya mwili wake wazi hafanyi kazi ngumu anpewa tuzo wakati mwanamke wa kijiji anataabika kama mjaa anavyosema anpigwa namume wake analisha familia na anavumilia asipewe tuzo kwanza kwa uvumilivu na pili kwa kujituma mnapeana wenyewe tu mjini! mi sioni faida. Hayo ni maoni yangu si lazima muyakubali
    Mrs. Jacob from kijijini

    ReplyDelete
  5. Nimependa sana ulivyobadilisha hii page ya maoni kaka Michuzi, keep it up!!

    ReplyDelete
  6. Kaka uliyetoa maoni yako hapo juu ni sawa kabisa, lakini wanasema kwamba ALIYE NACHO HUONGEZEWA BABAAA, KAMA HUNA HATA HICHO KIDOGO UTANYANG'ANYWA. Kwanza Ankal samahani maana Kilauea kukicha kuna sura za watu hazikosekani kwenye blog au ndio njia mpya ya utendaji kazi. Mtanisamehe kama Hali ya hewa imechafuka,lakini habari ndio hiyo.

    ReplyDelete
  7. Michuzi umeminya Koment yangu ambayo ilisistiza haya mawazo ya mdau namba moja hapo juu. Kina mama kule kijijini wanazalisha chakula kulisha nchi nzima, wanazalisha malighafi kwa viwanda vyetu, wanalea watoto katika mazingira ya taabu sana, wanachunga mifugo, wanavua samaki na shughuli kibao. Hao ndo wanahitaji tuzo na si hawa kina mama wa tabaka fulani hapa Dar es Salaam.
    Tafadhali Michuzi chapisha hii Komenti

    ReplyDelete
  8. WAKINA MAMA MLIOCHANGIA HOJA NA KUWAKUMBUKA WENZENU/WENZETU WA VIJIJINI NI SAWA KABISA MNAMAWAZO MAZURI NA YENYE KUWAJALI WWASIOKUWA NA UWEZO, MUENDELEE/TUENDELEE HIVYO KWA VITENDO. TUUMALIZE NA KUUFUTA UTAMADUNI WA KUJALI MASILAHI BINAFSI "UBINAFSI".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...