Marehemu Chembe enzi za uhai wake
Na John Kitime
Wiki ya misiba kwa jamii ya wasanii. Mwanamuziki wa kike ambaye kwa kweli alikuwa anakuja juu sana kiusanii Mwamvita Katundu anazikwa leo katika makaburi ya Kisutu Dar es Salaam saa 7 mchana. Mwamvita ambaye ni mke wa mwanamuziki wa Msondo Ngoma Juma Katundu alikuwa akiimba katika Bendi ya Bwagamoyo Sound inayoongozwa na Prince Muumini Mwinjuma.
Wakati huo huo, mwanamuziki wa muziki wa Kiasili aliyepoteza uwezo wake wa kuona miaka michache iliyopita, Chembe, au maarufu Mzee Bom kutokana na jina alilokuwa akitumia katika vipindi vya michezo ya redio, amefariki leo alfajiri katika hospitali ya Muhimbili baada ya kutokea matatizo ya kupanda kwa kisukari baada ya operesheni ya kibofu iliyofanyika Jumamosi. Taarifa zaidi za msiba wake zitatoka baadae.
Chembe aliwahi kuwa msanii wa kundi la Muungano, alikuwa na uwezo mkubwa wa kupiga ngoma nyingi kwa wakti mmoja hata baada ya kupoteza uwezo wa kuona, na alikuwa akilinganishwa na Mzee Nyunyusa. Niliwahi kupata bahati ya kufanya nae maonyesho Ujerumani mwaka 1994 wakati akiwa bado na uwezo wa kuona.
Mungu azilaze Roho zao mahali pema peponi - Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...