Wauaji wa Sudan striker Fredy ( Kushoto ) na kiungo Jaffar (kati kati ) ambao pia ni ma captain wa timu wakijadiliana mawili matatu wakati wa mapumziko ya mechi.
Time yetu ya Tanzania ikisali dua kabla ya mechi yao na Sudan ambayo ilijibiwa kwa ushindi
Timu ya Cameroon ikishangilia ushindi wao wa nusu fainali dhidi ya Nigeria
Kikosi kamili cha Tanzania kilichoizamisha Sudan kwenye nusu fainali katika picha ya pamoja.
Timu ya Sudan ambayo ilikua tishio hadi kushinda mabao 7 - 0 katika mojawapo ya mechi yake, ilitulizwa vyema na TZ na kufungwa mabao 2 - 0.

Timu yetu ya wa Tanzania wasomao Bangalore ilifanikiwa kuingia katika fainali za kombe la nchi za kiafrica zilizoko hapa Bangalore kwa kuifunga timu ya Sudan mabao 2-0.

Mashindano hayo yaliandaliwa na Umoja wa wanafunzi wa Kitanzania wasomao Bangalore( TASABA ) yalianza tarehe 26 february na yatafikia kilele chake leo Jumapili tarehe 6 March kwa mechi ya Fainali baina ya Tanzania na Cameroun, mechi ambayo itatanguliwa na Mechi ya mshindi wa Tatu kati ya Sudan na Nigeria.

Kwa habari na picha zaidi, tembelea
www.tasaba.net
au
www.tasaba.blogspot.com

Mungu ibariki Tasaba,
Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Africa...

UONGOZI TASABA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hongereni kwa ushindi lakini hizo jezi ndugu zanguni haziwakilishi Tanzania, kwanini msitafute rangi ya timu ya taifa? Au mmefanya mapinduzi mkiwa ughaibuni?

    ReplyDelete
  2. wabongo kwa kukosoa bwana, kwani kinachocheza mpira ni jezi au wachezaji?wapeni hongera watanzania wenzetu huko bangalore walau wamefika fainali sio kutoa makosa tuuu, ndio maana hatuendelei

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...