Ankal,
Hebu waonyeshe wadau,hali ilivyo Tambarare hapa nyumbani hasa wakati kama huu wa mvua.

Haya ni maeneo ya Milenium Tower Makumbusho kila mara Mungu anavyobariki kwa mvua basi huku kunakuwa tambarare na hata wafanya biashara wengine wanabidi wafunge biashara zao kwa maji kujaa maeneo yao hasa wanaotoa huduma za vyakula (Restaurant, Bar na Mama Ntilie

Mifereji ya eneo hili kila mara ni lazima izibe kutokana na eneo hili kuwa na watumiaji wengi bila kujali taka na maji machafu yanaelekezwa wapi.

Mdau.
Mc Kessy
Magari yalienda kwa mwendo wa pole katika maji yaliyojaa katika barabara.
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa mara tu baada ya kumalizika kwa mvua iliyonyesha leo jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...