Uongozi wa familia ya Liverpool unatoa shukrani sana kwa wapenzi na mashabiki wote waliojitokeza jana kwenye fiesta ya michezo pale Leaders Club jijini Dar, na kutoa pongezi maalumu kwa wachezaji wa kimataifa waliojitokeza na kuonesha kandanda safi iliyoacha gumzo kubwa.
Aidha, uongozi unatoa shukrani pia kwa waliojitokeza kuchukua fomu za uanachama na kujiandikisha pamoja na kuacha namba zao za simu na email ili kuendeleza umoja wetu ambao umekuwa mfano wa kuigwa na unaotupatia heshima kubwa kama watu wenye mipango thabiti.
Kwa wapenzi wa Liverpool waliokosa kufika jana Leaders Club ni kwamba mkutano wa dharura ulioitishwa uwanjani hapo umeafiki kwamba kuwe na mkutano wa wanachama wote siku ya sikukuu ya Mei Mosi yaani Mei 1, 2011 katika ukumbi wa Meeda Sinza, saa nane kamili mchana.
Pamoja na mambo mengine mkutano utajadili maendeleo ya familia ya Liverpool, usajili wa wanachama na kadhalika chini ya kauli mbiu yetu ya 'You Will Never Walk Alone'.
Hivyo shime wana familia ya Liverpool msikose kufika mkutanoni. Njoo ukiwa umevaa jezi ya Liverpool ili tupendeze na tuwe kitu kimoja. Matangazo zaidi yatakuja kupitia vyombo mbalimbali. Ukiwa na jambo piga simu hizo hapo juu na Website yetu inaandaliwa.
Asanteni Sana
Adam Gwao
Mwenyekiti

yap iyo safi sana wadau,tuko pamoja....YOU WILL NEVER WALK ALONE
ReplyDeleteYaani Michuzi kwa upendeleo!!!!! mbona Man U a.k.a timu ya dunia hujaitoa !
ReplyDeleteWewe mdau apo juu acha hizo. Wacha raha tujipe wenyewe. Kwani Man U hamna Ankal wenu?? Hahahaaaa limewashika na kama kawaida yenu mnaanza kuchonga hadi kwa Ankal wetu wa Bwawa la Maini. Ankal eeehhh... We bana asikwambie mtu nini wala nini. Kaza buti
ReplyDeleteU NEVA WOK ALONI
Wale Wacheza, Mashabiki na Wafadhili wetu Nyerere F.C msisahahu kuwa tutaanza mazoezi rasmi katika uwanja wetu wa Mugumu nyakati za jioni kuanzia mwezi ujao. Karibuni sana. Tutaendeleza ule mtindo wetu wa kuwachangia vijana wasio na ajira na walioko masomoni angalau wapate lishe bora na full gadgets za kuchezea.
ReplyDeleteHAPO WENGI FULANA FEKI - PIRATED
ReplyDelete