Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha (mbele) akiongoza wajumbe wa kamati ya utekelezaji CCM wilaya ya Iringa mjini na mkoa wa Iringa pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kukagua miradi ya utekelezaji wa Ilani ya CCM shule ya sekondari ya mazoezi Kleruu mjini Iringa
Katibu wa CCM wilaya ya Iringa mjini Charleys Charlesy akijibu kero za wananchi wa kijiji cha Nduli kutokana na diwani wa kata hiyo na mwenyekiti wake wa kijiji kutofautiana
Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi (kulia) na diwani wa kata ya Kihesa Mussa Wanguvu (kushoto) wakimwonyesha katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha (katikati) ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kihesa ,baada ya katibu huyo kutembelea kata hiyo jana kutazama utekelezaji wa Ilani ya CCM

Na Francis Godwin wa Globu ya Jamii,Iringa

CHAMA cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimetoa muda wa siku saba kwa mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Nduli, Ayubu Mwenda na diwani wa kata ya Nduli, Idd Chonanga kumaliza tofauti zao zilizoibuka baada ya kura za maoni ndani ya CCM mwaka 2010.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi wa kijiji hicho kulalamika mbele ya katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha kuwa kijiji hicho kwa sasa kimesimama kufanya shughuli za kimaendeleo baada ya viongozi hao kupingana wenyewe na pale mmoja anapoitisha mkutano ya hadhara mwingine huzuia wananchi kuwa hakuna kwenda katika mkutano .

Wakitoa malalamiko yao mbele ya katibu huyo wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa leo ,wananchi hao walisema kuwa toka kumalizike kwa uchaguzi mkuu mwaka jana kijiji hicho hakuna shughuli yeyote ya maendeleo ambayo imekuwa ikifanyika na chanzo ni diwani na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho ambao wamekuwa wakipingana.

Walisema kuwa hivi sasa wananchi wamekuwa wakiichukia CCM kutokana na viongozi hao kutofautiana na kuwa bado CCM imeshindwa kuchukua hatua zozote za kumaliza tatizo hilo .

Hivyo walitaka CCM kuwavua uongozi diwani na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho kutokana na kuendekeza makundi ya kisiasa na mivutano isiyomalizika.

Pia wananchi hao walisema kuwa katika kijiji hicho kumekuwepo na ufisadi mkubwa wa fedha za makusanyo ya mnala wa simu ,ardhi pamoja na kuwepo kwa kero kubwa ya maji na huduma za afya pasipo kushughulikiwa na viongozi hao ambao wamekuwa wakiendekeza malumbano zaidi.

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Iringa Charlesy Charlesy alisema kuwa CCM wilaya imepata kushughulikia kero hizo japo inashangazwa na hatua ya wananchi kuendelea kuibuka malalamiko zaidi.

Alisema kuwa chama ngazi ya wilaya kimefika mara kadhaa katika kijiji hicho kutatua malumbano hayo ya diwani na mwenyekiti wake .

Huku naibu meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki akiwataka viongozi hao kutenganisha siasa na utendaji katika kuwashughulikia wananchi hao .

“Mambo ya siasa yaende kisiasa na serikali yaende kiserikali wasichanganye mambo katika utekelezaji wa maendeleo ya kijiji cha Nduli…tengenezeni ratiba ya mikutano ya serikali “

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa ,Tesha alisema kuwa anatoa siku saba kwa viongozi hao kumaliza tofauti zao na kuvunja makundi ya uchaguzi na kama siku hizo zitamalizika bila kuvunjwa kwa makundi hayo kati ya diwani na mwenyekiti wake ambaye alikuwa mgombea katika kura za maoni nafasi ya udiwani ndani ya CCM basi chama kitachukua hatua dhidi yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mmegundua kwamba chama chenye demokrasia komavu kuliko vyote nchini ndicho chama pekee ambacho baada ya uchaguzi watu wanatakiwa "kuvunja makundi"?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...