Rais Jakaya Kikwete, akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Kilimo Dakawa , kilichojengwa na Serikali ya China kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Kilimo na wakulima vijijini ya matumizi ya teknolojia ya kisasa juu ya kukuza uzalishaji wa mazao na ufugaji leo eneo laDakawa , Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro.

Rais Jakaya Kikwete, akifunua kitanbaa kwenye jiwe la msingi kuashiria kuzinduliwa Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Kilimo Dakawa , kilichojengwa na Serikali ya China kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Kilimo na wakulima vijijini ya matumizi ya teknolojia ya kisasa juu ya kukuza uzalishaji wa mazao na ufugaji leo eneo laDakawa , Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro

Rais Jakaya Kikwete, ( watano kutoka kushoto) akioneshwa baadhi ya zana za kilimo yakiwemo matrekta makubwa na madogo baada ya kukizindua Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Kilimo Dakawa leo.

Rais Jakaya Kikwete, ( wapili kutoka kushoto) akiwa ameongozana na Mkewe , Mama Salma Kikwete ( kushoto) akiwa sambamba na Kaimu Balozi wa China hapa nchini , Fu Jijium ( watatu kushoto) sambamba na Waziri wa Kilimo , Chakula na Ushirika , Profesa Jumanne Maghembe ( wapili kutoka kulia) na RC Mkoa wa Morogoro , Issa Machibya ( wakwanza kuli) kwa pamoja wakiingiza rasmi katika Kituo cha Mafunzo ya Teknolojia ya Kilimo Dakawa leo.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwassa ( wapili kutoka kushoto) akibadilishana hoja mbalimbali na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika , Profesa Jumanne Maghembe , walipokuwa wakimsubiri Rais Jakaya Kikwete, kuzindua rasmi Kituo hicho leo

Ujumbe wa Serikali ya China ukiwa katika harakati za kupata picha nzuri za matukio ya kukizundua rasmi Kituo hicho. Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANANO "Dkt" Muheshimiwa J.Kikwete...HESHIMA YAKO....Hapatunatakiwa (tutengeneze na kuonyesha PEMBEJEO ZETU MADE IN TANZANIA)tuwe na bembejeo zetu TUBORESHE VIWANDA VYETU [fedha itunufaishe] other wise hii ni "CHUMA ULETE" kama "TUNAVYOKOPA NA KULIPA". KWAKIFUPI NI KWAMBA {WE MUST BE "SELFU RILAYANSI"}.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...