Waziri wa Maji,Prof. Mark Mwandosya akimkaribisha Mbeya mgeni wake, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Aliance For Green Revolusio in Africa (AGRA), Dr. KOFFI ANNAN pindi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mbeya.kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Mh. John Mwakipesile.Dr Annan akiwa mkoani mbeya atatembelea Taasisi ya ARI UYOLE na skimu ya umwagiliaji iganjo mbeya vijijini atatembelea Duka la pembejeo lusungo shamba la mahindi la mfano Mbozi atatembelea shamba la mfano la soya mbimba duka la pembejeo iyula na kuona bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kutokana na soya

Dr. Koffi Annan akiangalia ngoma ya asili ya kinyakyusa ifahamikayo kama lighoma pindi alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Mbeya.Dr Annan ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa AGRA (Aliance For Green Revolusio in Africa) inayojihusisha na masuala ya uboreshaji wa kilimo na utafiti katika nchi za Afrika
Watumishi wa benki ya NMB tawi la MBEYA nao walikuwepo kumpokea Dr. Koffi annan
Ngoma ya kinyakyusa ijulikanayo kama lighoma ikichukua nafasi yake wakati wa kumpokea Dr. Koffi Annan jijini Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. MWAMBIE AHAKIKISHE ANAPATA KIKOMBE KABLA HAJAONDOKA!!!

    ReplyDelete
  2. Hapo Kofi kapata mwenyeji wa ukweli! Yaani Mwandosya na Koffi kwa appearnce na usomi wanaendana kabisa!

    ReplyDelete
  3. HAKO KA AIRPORT KANATIA AIBU SERIKALI DOOOO

    ReplyDelete
  4. aaah sasa mbona mbunge wa mbeya mr sugu hayupo wakati wageni wamefika jimboni kwake au kila kitu ni usisiemu
    misupu usibane

    ReplyDelete
  5. Anonymous # 2,
    Waafrica mnakazania wasomi wasomi mbona mnashindwa kuiendeleza Africa na wasomi wenu? Wezenu akina Mark Zuckeberg(Facebook), Bill Gates(Microsfot), Michael Dell(Dell Copmuter) wamebadilisha dunia bila hata kuwa na degree moja.Mafundi baiskeli Wright Borthers wamebadilisha dunia kwa kutengeneza ndege bila hata kuwa na huo usomi mnaoupa kipaumbele. What about a farm boy Henry Ford?

    Amka kaka!

    ReplyDelete
  6. KingangitiApril 02, 2011

    Michuzi tafadhali huwa huweki maoni yangu mimi nikiandika ndo kwanza mada inafungwa sio vizuri ankal.Mimi napongeza sana jitihada za Mh.Waziri namwona ni mtu anayefanya mambo kwa uwezo mkubwa sana kt kila wizara anayogusa.The prof is very humble.kupata mawazo kutoka kwa wazoefu na wenye maadili kama hawa kina Koffi ni jambo jema na la maendeleo kwa Taifa.hongera kaza buti mhesh.waziri.

    ReplyDelete
  7. Mimi nimeona mambo mawili tu la kwanza wahusika wa Mkoa au uwanja wa ndege hayo maandishi juu ya bati si sahihi na ukichukulia watu toka nje wanapitia hapo neno sahihi ni AIRPORT na si AIR PORT. Jambo la pili ni ktk picha ya pili hilo bango la nguo neno la kwanza nalo si sahihi SUPPOPT usahihi ni SUPPORT, hivi hapakuwa na ukaguzi wa mambo kabla mgeni hajafika? Kumbukeni hizi picha zinakwenda mbali na ni aibu kwa Taifa
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...