Wananchi, viongozi mbalimbali, wabunge na wadau kutoka asasi mbalimbali wakifuatilia masuala mbalimbali kuhusu mchakato wa utaratibu wa kuandika katiba mpya ya nchi ndani ya ukumbi wa Pius Msekwa leo mjini Dodoma.
Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi katika eneo la ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma.
Wakazi wa Dodoma wakiwa wamejitokeza nje ya ukumbi wa bunge kutoa maoni yao juu ya mchakato wa kuanzishwa kwa mchakato wa utaratibu wa kuandika katiba mpya leo mjini Dodoma na kulazimisha kufungwa kwa muda barabara kuu ya Dodoma – Dar es salaam inayopakana na ukumbi huo.
Wananchi nje ya Bunge Dodoma leo
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. James Msekela akiongea na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa vurugu zilizotokea nje ya geti la ukumbi wa bunge leo mjini Dodoma. 

watanzania tutumie busara kwa kila jambo
ReplyDelete