Askari polisi wakingia eneo la stendi ndogo ya dala dala iliyopo kati kati ya mji wa Morogoro kwa ajili ya kuwatawanya wanafunzi waliozusha vurugu ya kuyazuia magari kupita barabarani kutokana na mgomo wa madereva wa daladala waliotaka kupunguziwa kwa ushuru wao wa sh: 300 kwa kila safari wanapotoka ndani ya stendi hiyo na kutaka ilipwe sh: 500 kwa siku , jambo lilolowakaasirisha wanafunzi kushindwa kwenda shule kufuatia mgomo huo Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari na Msingi katika Manispaa ya Morogoro wakijaribu kuyazuia magari kupita katika Barabara zinazoingia na kupita eneo la Stendi ndogo ya Daladala ya mjini hapa , kufuatia mgomo wa madereva wa daladala kusitisha kutoa huduma na wao kuathiriwa kwa kushindwa kwenda shuleni Hakuna kupita hapa mpaka kieleweke... Picha Gari ikiwa imepata kibano Baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari na Msingi katika Manispaa ya Morogoro wakijaribu kuyazuia magari kupita katika Barabara zinazoingia na kupita eneo la Stendi ndogo ya Daladala ya Morogoro Askari polisi waliokuwa wamezingira stendi ndogo ya dala dala iliyopo kati kati ya mji wa Morogoro kwa ajili ya kuwatawanya wanafunzi waliozusha vurugu ya kuyazuia magari kupita barabarani kutokana na mgomo wa madereva wa daladala waliotaka kupunguziwa kwa ushuru wao wa sh: 300 kwa kila safari wanapotoka ndani ya stendi hiyo na kutaka ilipwe sh: 500 kwa siku , jambo lilolowakaasirisha wanafunzi kushindwa kwenda shule kufuatia mgomo huo wakiondoa matairi yaliyowekwa njiani na wanafunzi Na John Nditi, Morogoro MAMIA ya Wanafunzi wa Msingi na Sekondari katika Manispaa ya Morogoro wamezusha mtafaruku mkubwa kwa kupambana na Polisi kwa muda wa saa nne ,huku wakiziba barabara wakitumia mataili mabuvu ya magari nawao wakijipanga katika barabara hizo kufuatia mgomo wa daladala zinazofanya safari zake ndani ya Manispaa. Sakata hilo lilisababisha Polisi Mkoani hapa kufyatua risasi baridi na nyingine za moto juu hewani kujaribu kuwatawanya wanafunzi hali ambayo iliwafanya kukimbilia kwenye makazi ya watu yaliyokua jirani ili kujificha na zahama hiyo. Katika mapambano hayo , Wanafunzi hao waliwatupia mawe ,mchanga na aina yoyote ya vitu walivyoviona mbele yao vinavyofaa kwa mapambano hayo kufuatiwa askari hao kuwazuia maandamano yao ya kwenda kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro , Issa Machibya, kuwasilisha kilio chao. Mtafaruku huo ulianza majira ya saa moja asubuhi jana ( Aprili 4) kwenye vituo mbalimbali vya kupandia daladala ikiwemo stendi kuu ya mabasi madogo iliyopo mji hapa na kusababisha maduka kadhaa yafungwe kwa muda baada ya madereva daladala kusitisha kutoa huduma hiyo wakilalamikia viwango vikubwa vya ushuruunaotozwa vyotozwa na Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro. Baada ya kukaa kwa muda katika vituo mbalimbali bila kupata huduma ya usafiri wa kuwafikisha mashuleni,wanafunzi walihamasishana kuchukua uhamuzi wa kukutana na wenzao katika stendi kuu ya daladala kujua hatma ya usafiri huo na ndipo walipoelezwa na madereva hao kuwa wamegoma kuingiza magari barabarani. Kufuatia jibu hilo wanafunzi hao walijikusanya na kuzuia barabara mbalimbali zinazoingia katikati ya mji ikiwemo ya Korogwe,Boma inayoenda Ikulu ndogo, Madaraka, barabara ya zamani ya kuelekea Dar es Salaam huku wakiweka mataili mabovu ya magari na kuyapiga zaidi magari ya Serikali na mashirika ya umma wakidai kuwa wameshindwa kutatatua kero hiyo. Sakata hilo pia lilikumba gari la Polisi la kikosi cha usalama barabarani lilokuwa likisambaza askari wake katika vituo mbalimbali vya kufanyia kazi huku wanafunzi hao wakionyesha jazba ya kuchukizwa na kitendo cha Serikali kushindwa kumaliza tatizo hilo madereva wa Daladala. Hata hivyo wanafunzi hao baada ya zoezi la kuzuia magari na kuyapiga kwa mawe huku wakisababisha msongamano katika barabara waliamua kuanza maandamano ya kwenda kwenye Ofisi ya Mkuu wa morogoro huku wakiimba nyimbo mbalimbali za kudai haki yao ya kwenda shule. Wakati wakielekea kwenye Ofisi hizo walipofika katika makutano ya barabara kati ya boma na sabasaba ndipo walipokutana na kizingiti cha Polisi wakiwa wamezuia barabara ya kwenda kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa morogoro. Baada ya kuona hivyo wanafunzi hao walimua kuokota mawe na kuwarushia askari hao ambao baadhi yao walijeruhiwa na mmoja wa waandishi wa habari walikuwa wakifatilia sakata hilo. Hata hivyo wanafunzi hao baada ya kuona askari hao wameondoka walijitokeza waliko jificha na kuendelea na maandamano hayo ndipo askari waliporejea kwa mara nyingine kupambana na wanafunzi hao na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya vinara wa maandamano hayo huku baadhi yao wakijeruhiwa kutokana na kuwakimbia askari. Wakizungumza na Waandishi wa habari kuhusina na hatua ya mgomo huo, katibu wa madereva wa Daladala, Hussen Lukwele, alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na Uongozi wa Manispaa kushindwa kulipatia ufumbuzi matatizo yao ya muda mrefu. Kwa mujibu wa Viongozi wa Madereva hao , kero kubwa ni la kupunguza ushuru wa sh: 300 kwa kila safari inayoanzia stendi na hivyo kulazimika kulipa wastani wa sh: 6, 000 kwa siku kiwango ambacho walidai ni kikubwa kulingana na mapato. Kero nyingi ambayo waliwasilisha katika Uongozi wa manispaa hiyo ni pamoja na stendi kushindwa kuhimili wingi wa daladala unasababisha baadhi yao kuegesha nje na matokeo yake zinakamatwa na Polisi na kutozwa faini kati ya sh: 50,000 hadi sh: 250,000 . Kufuatia hali hiyo ilimlazimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu, aliingilia kati na Kuitisha kikao cha dharura kati ya Uongozi wa Manispaa, Wakala wa usimamizi wa usafiri wan chi kavu na majini (SUMATRA),J eshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani na Viongozi wa Chama cha Madereva ili kutafuta njia muafaka ya kuwezesha kurejeshwa kwa utoaji wa huduma ya usafiri. Hata hivyo katika kikao hicho kulitokea mvutano kati ya viongozi wa upande wa madereva na uongozi wa manispaa kuhusu kiwango kinachopaswa kutozwa kwa siku ambapo manispaa walipendekeza sh: 1,000 kwa siku wakati madereva walitaka kulipa sh: 500 kwa siku kwa kufata vigezo walivyodai walishafanyia utafiti katika Jiji la Dar es Salaam. Wakati tofauti hizo zikijitokeza,Mkuu wa Wilaya hiyo alimuru Manispaa ikubaliane na pendekezo la madereva la kiwango chao kitumike kwa muda ili kurejesha huduma za usafiri kwa wananchi wakati suala hilo likiendelea kujadiliwa katika vikao vitakavyohusisha wadau wote wakiwemo na wamiliki wa daladala hizo. Kufuatia uhamuzi huo Viongozi wa madereva hao walikubali kurejesha huduma ya usafiri katika manispaa hiyo huku wakisubiri kikao hicho cha majadiliano zaidi ya pande zote zitakazofikiwa muafaka wa kudumu utakaowanufaisha wote. Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,Adolfina Chialo,alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kuna baadhi ya wanafunzi kadhaa wanashilikiwa kwajili ya mahojiano huku wengine wakifikishwa katika hospital ya mkoa kwajili ya kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa katika tafrani hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. " Chickens are coming to roost " ~ Malcom X

    ReplyDelete
  2. " Rise and rise till the lambs become the lions " ~ Robin Hood

    ReplyDelete
  3. inachekesha kweli..kila kukitokea maandamano ya wanafunzi,kutakuwa hakuna suluisho zaidi ni kuwapeleka akina ras makunja? si unaona picha ya chini yaani akina ras makunja hawana njia ingine wanayoijua bali ni...sebene la virungu? kazi hipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...