RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dk. Ali Mohemed Shein amemteua Nd. Abdulla Suleiman Abdalla kuwa mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu Mkuu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar Dk. Abdulhami Yahya Mzee, uteuzi huo umefanywa kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungo 5(3) cha sheria ya Chuo cha Utawala wa Umma nambari 1 ya mwaka 2007.
Kabla ya uteuzi huo Nd. Abdulla Suleiman aliwahi kuwa Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula (WFP) katika Wizara ya Kilimo ya Zanzibar, pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Mipango ya Mendeleo na Sera iliyokuwa Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar.
Nd. Abdalla Suleiman Abdalla ambaye ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha Utawala Umma Zanzibar anashada ya Chuo Kikuu.
Uteuzi huo umeanza Mei 25 mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...