Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais, akikagua gwaride la heshima wakati wa kufunga mafunzo ya uongozi katika chuo cha polisi huko Zanzibar
Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej akikaribishwa kukagua gwaride la heshima
Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej akikagua gwaride
Mhe. Fatma Abdulhabib Ferej akimvika cheo mmoja wa wahitimu
Mhe Fatma Abdulhabib Ferej alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya uongozi katika Chuo cha Zanzibar Police Academy Course No .1/2010/2011 kwa ngazi ya Koplo, Sajenti na Station Sajent. Mhe alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake ambapo jumla ya wahitimu 802 walimaliza mafunzo kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ,aidha Mhe Fatma aliwatuniku zawadi wanafunzi 6 waliofanya vizuri na kuonesha nidhamu na kuwavisha vyeo. Picha na mdau Othman Mapara


safi saana. hizi ndo zama za uhuru wa kuabudu.asiyeupenda atajiju.
ReplyDeleteHongera sana mhe. Fatma, Hivi na nyie mlikuwa mnaingia kwanza jkt kabla ya kujiunga na chuo kikuu, maana tulikuwa wote pale UDSM. lile suala la IDENTITY ZA VICHANGA wanapozaliwa hapo Zenji umeliboresha au umelisahau. Tuliliongea tulivyokutana Nairobi ukitokea Ghana.
ReplyDelete