Mwakalebela akitoka katika chumba cha mahakama na kulakiwa na mama yake mzazi (kulia) pamoja na wananchi wa Manispaa ya Iringa baada ya kushinda kesi yake kwa mara ya pili
Maofisa wa Takukuru mkoa wa Iringa wakiwa hawaamini kilichotokea leo mahakamani baada ya mahakama kwa mara ya pili kuitupilia mbali kesi ya Mwakalebela
Mwakalebela na mkewe Celina wakiwa kizimbani kabla ya kuachiwa huru na mahakama leo
Kwa mara nyingine aliyekuwa mshindi wa kura za maoni ndani ya CCM na aliyekuwa katibu mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela na mkewe Celina wameibwaga vibaya mahakamani taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa katika shitaka lao la kudaiwa kutoa rushwa wakati wa mchakato ndani ya CCM wa kutafuta ridhaa ya wana CCM kugombea nafasi hiyo.
Mbele ya hakimu wa mahakama ya Iringa Mh. Mary Senapee ,Mwakalebela na mkewe waliachiwa huru leo asubuhi baada ya kuonekana hawana hatia na hawana kesi ya kujibu katika shitaka hilo lililofunguliwa kwa mara ya pili ya Takukuru mkoa wa Iringa.
Mbele ya hakimu wa mahakama ya Iringa Mh. Mary Senapee ,Mwakalebela na mkewe waliachiwa huru leo asubuhi baada ya kuonekana hawana hatia na hawana kesi ya kujibu katika shitaka hilo lililofunguliwa kwa mara ya pili ya Takukuru mkoa wa Iringa.
Habari Kamili toka kwa Francis Godwin itafuata punde
Mwakalebela hakuwa anashindana na TAKUKURU! Hivyo kusema kwamba kaishinda si kweli. TAKUKURU imeshindwa kuthibitisha madai yake dhidi ya Mwakalebela. Zilizokuwepo ni TUHUMA TU! If this was a null hypothesis we'd say IT FAILED TO ACCEPT that Mwakalebela is guilty of...........
ReplyDeleteKilichotokea ni kwamba haki imetendeka.
Jamani nisaidieni ni Lini hawa Jamaa wa TAKUKURU tangu wakiwa TAKURU wameshinda kesi?
ReplyDeleteTatizo ni nini?
Hawana wataalam wa sheria?
Hawana ujuzi?
Wanafanya kazi kwa hisia badala ya utaalamu?
wanafanya kazi kwa msukumo wa kuambia kamata huyu?
Nadhani kuna haja ya kufutwa TAKUKURU
jamani naomba niwatetyee hao maofisa wa takukuru ni wanasheria tena nimesoma nao tumaini... poleni sana my collegemates.. pole sana kaka unanikumbusha mbali.... sio mbaya u have failled to prove beyond reasonable doubt this time.. usikate tamaa..... pongezi kwa mwakalebela
ReplyDelete