Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,pichani na waislamu wengine wakishuhudia harakati za mazishi ya Msanii Maarufu wa muziki wa Taarab,Maulid Mohamed Machaprala,aliyezikwa kijijini Bambi wilaya ya kati Unguja.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein,alishiriki katika mazishi ya Msanii maarufu wa muziki wa Taarab,Maulid Mohamed Machaprala,aliyefariki na kuzikwa leo kijijini Bambi,wilaya ya kati Unguja,pichani Dk Shein,akitia udongo katika kaburi kama ishara katika mazishi hayo.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,akishiriki na waumini wengine wa dini ya kiislamu kusalia Jeneza la marehemu Msanii Mzee Maulid Mohammed Machaprala,katika msikiti Nambar,Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Picha na mdau Ramadhan Othman wa Ikulu Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2011

    Mzee Maulidi kapumzike pema peponi.

    Kwa kweli tumeuona mchango wako kwa upande wa michezo ulipokuwa kijana na vile vile kwa upande wa muziki kama muimbaji mahiri.

    Nyimbo zako siku zote zitabaki kwenye mioyo yetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 14, 2011

    BurianiMohamed Maulid Machaprala, hakika kazi yako itabaki daima na itaendelea kuwa lulu.
    mungu ailaze roho yako mahali pema peponi.
    AMIN

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 15, 2011

    Huyu alikuwa goakeeper mahiri enzi za Challenge Cup, Africa Mashariki nzima alitamba ndio maana akapewa hili jina la Machaprala, sio jina lake ni la kimichezo. Wenye picha za Challenge timu ya Zanzibar hebu tutoleeni humu kwenye globu, Usanii na michezo ni asili ya ukoo wao lakini ni wajasiriamali maarufu pale zanzibar, maana ukoo wao ni maseremala nafikiri hata watoto wao wamerithi. Ah! ardhi inachukua watu. Kaalu inna lillahi wainna ilayhi raajijun

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...